Vita Iran: Trump awaita washirika wa NATO “waoga”

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph, Imechapishwa : March 20, 2026 17:33 (EAT)

Vocalize Pre-Player Loader

Rais Donald Trump amewaita washirika wa NATO “waoga” baada ya kushindwa kupeleka wanajeshi kwa ajili ya kuufungua Mlango Bahari wa HormuzPicha: Annabelle Gordon/AFP

Trump amewaita washirika wa NATO “waoga” baada ya mataifa mengi ya Ulaya kukataa kutuma vikosi vya majini kulinda Mlango-Bahari wa Hormuz. Israel imesema inaendelea kushambulia “miundombinu” huko Tehran. DW ina zaidi.

Unachohitaji kujua

Unachotaka kufahamu:

  • Trump ‘awananga’ washirika wa NATO kwa kushindwa kumsaidia vitani
  • Walinzi wa Mapinduzi wa Iran wameripoti kwamba msemaji wao ameuliwa katika shambulizi la anga.
  • Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Kuwait zimejitokeza kujibu mashambulizi ya makombora.
  • Israel inaendelea kulenga ‘miundombinu’ mjini Tehran, lakini imesema itajizuia kufanya mashambulizi zaidi katika kiwanda muhimu cha gesi.
  • Kyiv yatuma vikosi vya jeshi Mashariki ya Kati kudhibiti droni za Iran 

Iran yasema itawalenga maafisa wa Marekani na Israel katika ‘maeneo ya burudani’

Msemaji wa jeshi la Iran amesema kwamba Tehran inaweza kuwalenga maafisa na wanajeshi wa Marekani na Israel katika maeneo ya starehe na ya kitalii.

Msemaji wa jeshi, Abolfazl Shekarchi alinukuliwa na shirika la habari la Mehr akisema kwamba Iran inawafuatilia ‘maafisa wa adui, makamanda, marubani na askari,’ na kuongeza kuwa ‘maeneo ya starehe, vivutio vya utalii na vituo vya burudani’ hayatakuwa salama tena.

Marekani na Israel wamewaua maafisa kadhaa wa ngazi ya juu wa Iran kupitia mashambulizi ya angani, akiwemo Kiongozi Mkuu Ali Khamenei na hivi karibuni mkuu wa usalama Ali Larijani.

Mnamo Ijumaa, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi la Kiislamu (IRGC) limesema kwamba msemaji wao, Ali Mohammad Naini aliuliwa katika mashambulizi ya Marekani na Israel.

Trump awaita washirika wa NATO “waoga” kwa kushindwa kusaidia vita vyake na Iran

Rais Donald Trump aliwashambulia washirika wa NATO siku ya Ijumaa kwa kushindwa kumuunga mkono kwenye vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran, akiwaita washirika hao wa muda mrefu wa Marekani kuwa “waoga.”

“Bila Marekani, NATO NI KAMA CHUI ASIYE NA MENO!” Trump aliandika katika chapisho kwenye mitandao ya kijamii.

Rais wa Marekani alilalamika kwamba nchi za NATO hazikutaka kujiunga na vita dhidi ya Iran, lakini bado zinalalamika kuhusu bei kubwa za mafuta.

“Sasa kwa kuwa  kijeshi, bila hatari kubwa kwao, wanalia kuhusu bei ya juu ya mafuta wanazolazimika kulipa, lakini hawataki kusaidia kufungua Mlango Bahari wa Hormuz, hatua rahisi ya kijeshi ambayo ndiyo sababu kuu ya bei hizo za juu za mafuta. Rahisi sana kwao kufanya, bila hatari kubwa,” aliandika.

“WAOGA, na TUTAKUMBUKA!”

Onesha maudhui ya nyongeza?

Maudhui haya ni sehemu ya matini unayoyasoma. Mtumaji X / Twitter anatoa maudhui haya na anaweza kukusanya data za matumizi moja kwa moja unapobonyeza “Onesha maudhui”.Daima onesha maudhui kutoka kwa X / Twitter

Kyiv yatuma vikosi Mashariki ya Kati kudhibiti droni za Iran — afisa wa ulinzi wa Ukraine”

Ukraine imetuma vikosi vya kijeshi katika nchi kadhaa za Mashariki ya Kati kusaidia kukamata ndege zisizo na rubani, amesema afisa mwandamizi wa ulinzi wa Ukraine, Rustem Umerov.

Katika chapisho kwenye X, Umerov alisema alitembelea Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Saudi Arabia, Qatar na Kuwait, pamoja na Jordan na kwamba Kyiv imetuma vikosi katika nchi hizo.

“Wataalamu wa kijeshi wa Ukraine wanafanya kazi katika kila moja ya nchi hizi chini ya uratibu wa Baraza la Usalama wa Taifa na Ulinzi,” alisema.

“Vikosi vya kukamata droni vimetumwa kulinda miundombinu ya kiraia na ile muhimu. Kazi ya kupanua maeneo ya ulinzi inaendelea.”

Umerov ni katibu wa Baraza la Usalama wa Taifa na Ulinzi la Ukraine, chombo kinachojumuisha Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, mawaziri kadhaa na maafisa wengine waandamizi.

Jeshi la Ukraine lina uzoefu wa kuangusha droni za Iran aina ya Shahed, ambazo zimekuwa zikitumiwa na Urusi tangu ilipoivamia Ukraine Februari 2022.

Tehran imelenga maeneo katika nchi za Ghuba ya Uajemi kujibu mashambulizi ya mabomu ya Marekani na Israel nchini Iran.

Msemaji wa Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi auawa katika mashambulizi ya Marekani na Israel, Iran yasema

Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi la Kiislamu la Iran (IRGC) kimesema kwamba msemaji wao, Ali Mohammad Naini, ameuliwa katika mashambulizi ya Marekani na Israel, hatua inayoongeza idadi ya vifo vya maafisa wa ngazi ya juu kwenye mzozo huo.

Naini ‘alifariki shahidi katika shambulizi la kigaidi, kikatili na la woga lililofanywa na Marekani na Wazayuni alfajiri,’ Walinzi hao walitangaza kupitia tovuti yao ya Sepah News.

Vyombo vya habari vya serikali ya Iran pia vimeripoti kwamba Naini, ambaye amekuwa msemaji wa IRGC tangu 2024, aliuliwa wakati wa mashambulizi hayo, ingawa bado hakuna uthibitisho wa haraka kutoka Israel au Marekani.

Ufaransa ‘kuendelea na msimamo wake’ kuhusu Ukraine licha ya vita vya Iran — Macron

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema kwamba Paris haitapunguza msaada wake kwa Ukraine baada ya kuzuka kwa vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

‘Tunaendelea na msimamo wetu,’ Macron alisema kupitia chapisho kwenye mtandao wa X.

‘Vita nchini Iran havitaifanya Ufaransa kuiacha Ukraine, ambako uvamizi wa Urusi unaendelea.’

Amesema kwamba jeshi la wanamaji la Ufaransa lilikamata meli katika Bahari ya Mediterania iliyoshukiwa kuwa sehemu ya meli ‘kivuli’ za Urusi zinazotumika kukwepa vikwazo vya kimataifa.

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatar Norrbottens lanrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islands

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,344 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply