Imeandikwa, “Lakini hawatakuwako maskini kwenu; (kwa kuwa Bwana atakubarikia kweli katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako, uimiliki, iwe urithi wako;). ( Torati 15:4).
Ahadi ya Mungu kwa wacha Mungu wake ni kuwatajirisha kupitia baraka zake. Mungu anatupatia fursa ya kuwa matajiri ili kutupa uhuru wa kiuchumi ambao ndiyo uhuru kamili katika ulimwengu huu tuliyopo.
Hata ukiwa na upako mkubwa kiasi gani, au karama kubwa kama wewe ni maskini itakuwa ngumu sana kwako kuheshimiwa na jamii inayokuzunguka hapa duniani hata mbinguni pia.
Maana heshima ya mtu ipo katika uwezo wake wa kiuchumi, huu ni ukweli usiopingika, hata kama tutajidai kuweka misemo kwamba binadamu wote ni sawa..
Just imagine, wewe ni mchungaji uliyeokoka na unampenda Yesu kweli kweli, lakini wakati wa changizo la ujenzi wa kanisa au ununuzi wa vyombo vya huduma unaandika barua ya kuomba pesa kwa wanasiasa au wafanyabiashara ambao wengine sio walokole kama wewe pengine ni washirikina lakini kwa sababu wana pesa inakubidi uwe mpole, uwabembeleze na kuwapamba kwa maneno matamu ili wakusaidie kutimiza maono yako. Hii inatokana na umaskini na siyo kukosa Roho wa Mungu au kupungukiwa na mistari ya biblia kichwani.
King Solomon katika zama zake aliwahi kuiongelea hali ya umaskini, akasema, “Hekima ya maskini hudharauliwa, wala maneno yake hayasikilizwi”. (Mhubiri 9:16).
Maskini hata akiwa na hekima bado umaskini wake unaweza kuwa kikwazo cha kumkosesha fursa mbele ya jamii, maana fungu la umaskini lipo katika kudharauliwa tu.
Bwana Yesu amewahi kutoa mfano juu ya maskini mmoja aliyejulikana kama Lazaro, biblia inasema, maskini huyo alikuwa mcha Mungu sana hapa duniani, na baada ya kufa pamoja na umaskini wake akafanikiwa kuingia mbinguni.
Jambo la kushangaza, baada ya maskini huyu kuingia mbinguni alionekana amepakatwa na kulalia kifua cha tajiri mmoja anaeitwa Abrahim, na akiwa huko huko mbinguni tajiri mwingine aliyekuwa jehanam akawa anamuomba Abrahamu ampe ruhusa huyo maskini aende motoni ili kumuhudumia kinywaji.
Yaani ameingia mbinguni lakini kwa ajili ya cv yake ya umaskini wa duniani inasababisha adharauliwe tena akiwa huko huko mbinguni, mbaya zaidi anadharauliwa na mtu aliyeko motoni na kumuona kama vile muhudumu wa bar.
Vijana wenzangu na wakristo wenzangu tutafuteni pesa ili tukifa tuingie mbinguni tukiwa matajiri, ili kuepuka kupakatwa na wanaume wenzetu waliomcha Mungu na kutengeneza pesa kipindi wako hapa duniani.
Hata tuimbe mapambio na kuhubiri kwa kiasi gani kama tukifa tukiwa maskini tutadharauliwa hadi mbinguni na kuonekana kama wahudumu wa vinywaji tu…
Kama ahadi ya Mungu kwenye maisha yetu ni kututajirisha….. Let us work hard and make money ili tusiingie mbinguni kinyonge kama Lazaro…..
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.