Unaweza endelea kutia bidii.

Usikubali mtu yeyote aamini kuwa hauwezi kufanikiwa bila yeye. Maana imeandikwa, “Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana”. (Yeremia 17:5).

Ni kweli ili tufanikiwe tunahutajiana ila siyo vyema hitajio hilo likaiondoa nafasi ya Mungu kwenye moyo wa mtu.

Ukiona umeachwa na mtu kimahusiano, kihuduma, kibiashara nk na ukahisi uhai wako hauna thamani tena bila uwepo wa mtu huyo kwenye maisha yako, jua kuwa umeanguka katika imani na uko karibu na kupotea, unapaswa kutubu mara moja na kumrudia Mungu ambaye yeye ndiye ngome na fahari yetu.

Wapo watu wanakusapoti kihuduma au kimaisha na wamefanyika msaada mkubwa kwako, majira yao ya kuwa na wewe yaki expire waache waondoke, usiwalilie, usijidhulu kwa ajili yao, kubali kustahimili maumivu yako na kuyakabidhi kwa Mungu kisha songa mbele na safari yako.

Kuwang’ang’ania, kuendelea kuwalazimisha wawepo kwenye maisha yako hiyo ni dalili ya kutomuamini Mungu na ndiyo tafsiri sahihi ya ibada ya sanamu.
Let it go, start your new life, najua kuna gharama ya kuanza upya ikiwemo gharama ya kuchekwa, kudhihakiwa, kuonekana hauna maana kwenye jamii yako, lakini ni vyema gharama zote hizo ukazielekeza msalabani maana hapo ndipo tunapatia nguvu ya kuanza upya.

Wala usiwachukie watu waliosababisha maumivu yako maana Mungu amekuandalia shuhuda njema na promotion kubwa juu ya hicho unachokipitia.

Nb: Nguvu zetu zinapatikana katika madhaifu. Ushindi wa Yesu ulipatikana baada ya kuteswa, kusulibiwa hadi kufa, mifupa ya Elisha ilifufua, Yusufu alikumbukwa akiwa gerezani.
Muhimidi Mungu hata katika magumu na madhaifu unayopitia maana kwake kuna faraja ya milele.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment