Matendo ya Mungu ni fumbo kubwa kwetu.

CantonaCast Television- No 1 Online Television Discover the Difference

Maandiko yanasema, “Mambo ya siri ni ya Bwana, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele” (Torati 29:29). Na tena Paulo akaandika, “Hukumu za Mungu hazichunguziki wala njia zake hazitafutikani” ( Warumi 11:33). Maneno haya yanaonyesha kuwa matendo ya Mungu kwenye maisha yetu huwa ni fumbo kubwa.
Inahitajika neema ya ajabu sana kuielewa lugha ya Mungu pamoja na nia yake maana hakuna ajuae kile anachokiwaza au anachokipenda.
Hebu tazama hili, katika sheria ambazo Mungu alimpatia Musa alimkataza kabisa swala la waisraeli kuoa wanawake wa mataifa mengine (Torati 11:2-4), lakini baada ya miaka mingi baada ya Musa tunakuja kuona Samsoni ambaye ni mnadhiri wa Mungu anapendana na wanawake wa kimataifa, wafilisti. Na jambo hili linaonekana baya sana machoni kwa wazazi wake maana siyo tu anawakosea wao bali anayavunja hata maagizo ya Mungu, lakini maandiko yanafafanua kuwa, ni Mungu aliyaruhusu hayo ili aweze kupata sababu ya kuwalipa kisasi wafilisti (Waamuzi 14:3-4).
Kwa maana hiyo, makusudi ya Mungu ili yatimie ndani ya wito wa Samson ilibidi kwanza apitie mazingira ya kutoeleweka kwenye jamii yake na kuonekana muasi juu ya maagizo ya Mungu. Kwa wakati huo binadamu waliona makosa ndani ya maisha ya Samson, lakini Mungu akayaona makosa hayo kama njia ya kumfikisha Samson katika hatima ya wito wake. Inawezekana wapo walimkatia tamaa hata kufikia hatua ya kutilia mashaka wito wake, lakini Mungu alikuwa anaona ushindi kupitia kile kisichoeleweka ndani ya jamii ya Samson. Hii imenifundisha kuwa kuiga mtindo wa maisha ya watu fulani ili uweze kueleweka na jamii yako inaweza kuwa ndiyo sumu ya kuua ndoto zako pasipo wewe mwenyewe kujua, bali ukiishi maisha yanayoendana na makusudi ya Mungu juu ya wito aliyokuitia inakupa nguvu ya kushinda vikwazo na kuifikia hatima hata kama jamii yako haitakuelewa kwa wakati huo. Kama inabidi kuwa mkali ili ndoto zako zitimie, usije kuigiza tabia ya upole maana hiyo itakuulia ndoto zako.
Kuwa jinsi ulivyo kwa kukubali gharama ya kuchukiwa, kukataliwa, kufitiniwa nk, ili mradi tu ubakie kuwa halisi kama Mungu anavyotaka uwe.Je ni mme wako amekukana,ni Mke amevunja mahusiano yenu,ni marafiki wamekutotoka,ni biashara yako imesambaratika,umefutwa kazi ni lipi Hilo ambalo unalipitia mwaka huu.Ni fumbo endelea kumtazama Kristi mambo mazuri yanakudubiria.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment