CantonaCast Television- No.1 Online Television Discover the Difference
Kuna watu wapo katika maisha yetu kwa ajili kutukomaza ila sio wa kuwangangania na kuwashikilia inabidi waondoke tuu ili walio sahihi wachukue nafasi yao
Maandiko yanasema alipokufa uzia nalimuona Bwana huyu ni isaya alitambua kuwa Uzia alikuwa kwazo la yeye kumuona Bwana,kuna watu lazima waondoke kwa njia yoyote ili amani,furaha,super love na faraja za mioyo yetu ipatikane (let them go)
Naomi alikaa na wakwe zake wawili Ruth na Oprah kwa miaka 10 alipoona aridhi ya Moabu inamtesa imeuwa watoto wake wawili na mume wake na mali zake alipoamua kwenda Bethlehem kwa sababu kulikua na neema Ophra alikataa kwenda naye
Hiyo haikumvunja moyo kwa kile alichokiamini aliona ni bora amuachie Oprah aende zake lakini yeye afike kwenye hatima yake
Tusiumie wanapoondoka maishani mwetu maana wanatupa nafasi ya kutimiza ndoto zetu kwa kujiamini zaidi (let them go)
Hofu sio kupenda hofu ni kuishi na mtu asiyekupenda.
Hofu sio kushare Naye sex bali hofu ni kushare naye ideas zilizoshikilia hatima yako.
Hofu sio kuishi naye bali hofu ni kupoteza muda wa kuwa naye
Sijaumia kuachana naye ila nimeumia kuchelewa kuacha naye (let them go)
Ikiwa baba na mama yako walikupenda na kuwekeza mengi maishani mwako wameenda na ukalia, kutoa machozi na ukafuta machozi ukaanza upya bila wao pls amekumiza sana,amekutoa machozi sana,amekurudisha nyuma sana na hajui umuhimu wako achana naye. Anayekudharau na unanipenda si mpenzi wa kweli,ipo siku atafahamu umuhimu wako.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.