Njaa ni mbaya

CantonaCast Television- No 1 On-line Television-Discover the Difference

Njaa ni mbaya sana, tena sana. Siku zote njaa ndiyo sababu ya watu wengi hata kukosea na kumkosea Mungu.

Njaa ndiyo sababu ilimpelekea Yesu kuulaani mtini (Marko 11:13-14).

Njaa ndiyo sababu iliyompekea Daudi kula mkate wa uonyesho, jambo ambalo halikuwa halali kwake yeye na wenzake aliokuwa nao (1 Samweli 21:3-6/Luka 6:3-4).

Njaa ndiyo sababu iliyompekea Ibrahim akimbilie Misri, nchi ambayo ilimgharimu hata kumkana mke wake (Sara) na kumtambulisha kama dada yake akihofia asije kufa kwa makali ya upanga ya watu wa Misri (Mwanzo 12:10-15).

Njaa ndiyo iliyosababisha mavi ya njiwa na vichwa vya punda kuwa chakula kinachouzwa kwa gharama kubwa sana katika nchi ya Israel mji wa Samaria kwa takribani miaka mitatu, (2 Falme 6:25)

Njaa ndiyo iliyopelekea mwanawake mmoja wa Samaria kukosa huruma na kumgeuza mtoto wake wa kuzaa kuwa chakula na kumnywa supu katika kipindi cha Elisha, (2 Falme 6:28-29).

Katika maisha ya kawaida pamoja na utumishi njaa ndiyo imekuwa sababu kubwa ya watu wengi kukosea. Katika maombi yako siku zote hakikisha sehemu ya maneno unayoyatamka ni kumwomba Mungu akuepushe wewe na familia yako na njaa ili isije kuathiri uaminifu wako katika utendaji wa taaluma uliyo nayo na kukuharibia sifa yako katika utumishi au maisha yako.

Ni maombi yangu na dua Mungu akupe utoshelevu katika maeneo yote ya maisha yako ili uweze hata kumtumikia huku ukiwa hauna uhitaji wa tumbo lako…


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment