Ninaamini Mungu Amekuwa Mwaminifu kwenye maisha yako. Hata kama bado unasita rohoni kukubali Uaminifu WA MUNGU na bado unajiuliza kama Ni Mwaminifu Kwako bado nina nafasi ya kukujulisha juu Uaminifu Wake kwako.
Mungu Anakupenda, hakupendi kikawaida Anakupenda Upeo. ANAKUPENDA UPENDO WA AGAPE.
Pumzi unayovuta… na the fact kwamba unaishi wapo wenye matatizo kuliko wewe.
Je unapitia magumu? Je unahisi umeachwa? Je unahisi una laana?
Jibu ni jepesi… usitafute mchawi.. jitazame mwenyewe.
Si kila anayepitia magumu basi ana dhambi wengine ni mapito kwa ajili ya maandalizi ya huko mbele Ambako Mungu Amekuandaa.
Unadhani kwenye Tatizo Lako Mungu Hayupo na Wewe? Kumbuka kwenye Tundu la Simba Daniel hakuwa peke yake,
Kumbuka kwa Shedrack, Meschack ana Abelnego Yesu Alikuwa nao Motoni mpaka Nebuchadnezzar akasema mbona nawaona sasa ni wanne? Na mmoja ni mfano wa wana wa miungu? Je hatuwatupa watatu? Mbona nawaona wanne? Daniel sura ya 3
Ni Mungu Yesu Alikuwa nao hata kwenye pito la moto.
Angalia Yusufu yupo Gerezani na Biblia inasema kwamba Mungu Alikuwa pamoja naye Gerezani… can u imagine? Gerezani naye Anakuja kukaa na wewe Gerezani..
Je upo mazingira gani? Hauna ada? Hauna mume? Hauna kazi? Unapitia mateso?
Wengine wamejaribu kuhama Makanisa wakidhani ndio solution kumbe solution ni kutulia Miguuni Pa Yesu.
Soma hii
Mwanzo 39:21
Lakini BWANA akawa pamoja na Yusufu, akamfadhili, akampa kibali machoni pa mkuu wa gereza.
Vile vile kumbuka na Tazama Biblia inasema…
1 CORINTHIANS. 16:22
Mtu awaye yote asiyempenda Bwana, na awe amelaaniwa. Maran atha.
LAANA IPO KWA ASIYEMPENDA BWANA. Sasa najua wewe ni mtu mzuri Unayempenda Bwana Yesu. Endelea kuvumilia.
Biblia Inasema kila jaribu linakupata ni kipimo chako cha Kawaida na Kupitia Uaminifu Wa Mungu Basi Atafanya Mlango wa Kutokea.
Kumbuka Mungu Atafanya Mlango Siyo wewe kuanza kutafuta Mlango hapa ndipo penye mtego wengi wametafuta mlango kwa njia zao wakajuta baadae..
Soma hapa
1 CORINTHIANS 10:13
Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.
Wakristo wengi tuna tabia ya kutafuta mlango wa kutoka kwenye majaribu na tunaishia kubaki gerezani kwa muda mrefu…
Ilimlazimu Yusufu Mwaka Mmoja zaidi wakati amemtafsiria mtu ndoto Gerezani kisha akaomba msaada kwa Mwanadamu amkumbuke akirudishwa kwa Farao Biblia inasema alipotoka Gerezani yule mtumishi wa Farao Alimsahau Yusufu najua sababu ya kumsahau ni Mungu Aliruhusu ili Yusufu Tumaini lake libaki kwa Mungu.
Kasome Biblia yako..
MWANZO 40:14, 21, 23
Ila unikumbuke mimi, utakapopata mema, ukanifanyie fadhili, nakuomba, ukanitaje kwa Farao, na kunitoa katika nyumba hii. Akamrudisha mkuu wa wanyweshaji katika kazi yake ya kunywesha, naye akampa Farao kikombe mkononi mwake. Lakini huyo mkuu wa wanyweshaji hakumkumbuka Yusufu, alimsahau.
Haijalishi hali uliyonayo naonba ujue ya kuwa YESU ANAKUPENDA SANA na wewe ni wa thamani, isemeshe nafsi yako ambayo haitaki kukubali kuwa Yesu Anakupenda,
Daudi alikua anaisemesha nafsi yake kila inapotaka kuinama…
Eeh Nafsi yangu kwa nini kuinama? Umuhimidi Bwana… jitie nguvu kwa Bwana Yesu Mpendwa Wangu.
Kasome Zaburi ya 42 na 43 kila saa anaisemesha nafsi. Nafsi ina tabia ya kuchoka ina tabia ya kutaka raha za dunia nje ya wakati, ukiishinda nafsi umeshinda tamaa na matarajio ya mwilini.. kisha unabaki Katika Makusudi ya Mungu.
Warumi 8:35
Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?
Haijalishi unapitia yapi leo, haijalishi kama umerudi nyuma kuna tumaini.. Yesu ni TUMAINI, Yupo Yesu Wa nafasi ya pili Mungu wa Second Chance yupo.. hakika Yupo kuna kuinuka Tena.
Je umechoka kabisa unahitaji maombi?
Nipo kwa ajili yako lakini pia nchi hii ina watumishi wengi wazuri pia unaweza tafuta Mtumishi Unayemuamini tushikane mkono kuutafuta Uso wa Mungu kwa Pamoja na hakika Atakuonekania.
Distance is not a barrier.
Haya njooni Tusemezane Asema Bwana…
Isaya 1:18
“Njooni basi tuhojiane,” asema Bwana . “Ingawa dhambi zenu ni kama rangi nyekundu, zitakuwa nyeupe kama theluji; ingawa ni nyekundu sana kama damu, zitakuwa nyeupe kama sufu.
Una ugonjwa usiopona? Una tatizo sugu? YESU YUPO ANAJUA SHIDA ZAKO.
Ufunuo 3:20
Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.