Mazingira uliyomo yasikuvunje moyo.

Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu,hachagui atakapozaliwa au wazazi,hana uwezo kubaini atazaliwa bara hili au lile,tabaka hili au lile,mzungu au mwafrika.Wazazi wametwikwa jukumu kubwa kulea watoto katika misingi ya madili mema,mienendo Bora huku wakizingatia umuhimu wa kupenda Mungu aliyewaumba maishani.Ni jukumu la mzazi yeyote yule kuekeza katika elimu ya mtoto wake na kufuatilia anaendelea vipi masomoni maana ni ufunguo wa maisha ya kesho.Mazingira mtoto amezaliwa ndani yasimnyime nafasi ya kufikia ndoto yake maishani.

Wazazi wakiwa walezi wa kipaji cha mtoto ni jukumu lao kutambua huyu mtoto anakipaji kipi Mungu alichompokeza kipalilie mapema.Mataifa yaliyoendelea yameratibu umuhimu wa kulea kipaji cha mtoto akiwa umri mdogo.Mtoto akiwa na umri umri wa siku Hadi miaka mitano ana uwezo kujifunza lugha tofauti na kunasa mambo mengi ambayo yanajenga msingi wa maisha yake.Miaka mitano hadi kumi na minane,ni msimu atanyoka akiwa na misingi mizuri ana ataharibika iwapo hatapokea maelekezo. Iwapo samaki hujamkunja akiwa mbichi je?utamkunja akiwa amekauka.Wazazi wengi wamepoteza dira kutilia maanani ukuaji wa mtoto,kipindi miaka ya mwanzo baadae wanakumbana na mlima wa magumu,wanapojiusisha na vikundi vinavyo badili mkondo wao wa maisha. Iwapo wewe mzazi mzembe,huna utaratibu unapopanga mambo.Je unatarajia mtoto kujifunza nini? Wewe hauendi kanisani je unatarajia mtoto huyo aende kanisani? Unaenda na mwanao kilabuni,unarejea nyumbani, umelewa unagombana na mkeo,nyumbani hamna amani,je kesho atayafanya hayo hayo.Hiki ni kizaza kinaiga na baadae kitakumeza wewe mzima. Mzee mmoja kijijini mwetu alikua tajiri saana,alijaliwa watoto wawili wa kiume,aliwapa walichotaka maishani, lakini walikua wazembe Sana.Alipo ugua na umri umekwenda,alihisi mda wake duniani unakamilika,alikosa usaidizi kutoka kwa watoto wake,walimtelekeza.Siku moja jioni aliandaa kikao na wanawe akawafahamisha maisha ni mafupi mno na karibuni atasafiri kuungana na wazee walio mtangulia.Aliwapa historia alivyo zaliwa katika maisha ya uchochole,alitia bidii masomoni,wazazi wake waliangaika wapate mlo wa siku na wao wapate elimu.Alijifunza umuhimu wa kuekeza akajenga jina lake kulifikisha lilipo Ilikua kazi ngumu mfano kupanda mchongoma,Mzee yule iliwapa usiku ule wanawe uridhi, aliwatakia heri maishani.Kabla kikao kukamilika aliwagawia vipande vya ardhi alivyonunua na stakabadhi mahala zipo.Siku moja asubuhi alisikia wanawe wakigombana, nyumba ni yangu,naye wa pili anafoka,tatizo aliloliona kitambo maana hamna aliyejibidihisha kujenga yake.Aliandaa kikao cha pili akawafahamisha atakapo fariki dunia amewandalia hazina ya fedha saduku lipo chini ya msingi wa nyumba yake nzuri. Mzee yule tajiri alifariki dunia. Ibada ya mazishi ilifanyika,mwanasheria akadhibitisha Mzee yule aliandaa mambo yake kwa utaratibu na wanawe wakaridhia hilo.Baada ya miezi mitano,wanawe wakakubalia kuchimbua kwa utaratibu kutafuta hazina.Nyumba iliporomoshwa kutafuta saduku la fedha walichokumbana nacho ni karatasi yenye mandishi wanangu iwapo nyinyi ni wanaume basi jengeni nyumba yenu kila mmoja kubwa hata kushinda hii niliyojenga pasipo usaidizi wa wazazi wangu maana mna heri nyie mna viwanja mimi baba yenu sikuridhi chochote kutoka kwa wazazi wangu.Walichonipa ni elimu na hekima Mimi nimewapa vyote viwili. Nyumba ilikua imeporomoka hawana misingi ya kujenga nyumba.Ni wavivu hawajui ukulima,hawana fedha,hawana mtaji,si wajasiriamali,viwanja vilipigwa bei usiku na mchana.Hebu niseme hivi,mzazi ni jukumu lako kusimulia maisha uliyopitia maishani unapoketi kivulini mbeye ya watoto wako,palilia misingi ya kutafuta,wasisubiri wapokezwe.Maana miaka ya alafu itakua ya taabu sana iwapo watasubiri mfupa uteleze mikononi mwako.Wafahamu safari yako maishani na watilie mkazo kufanya kazi kwa bidii wajijenge sifa wenyewe, utakuwa tuu,mshauri wao kusaidia wafikie azma yao maishani hakika ukipanda pantosh utavuna pankwisha.Maisha ni Mafupi.

#Iposiku #Getinspired #CantonaJosephMotivates


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment