HUDUMA ALIYOKUPA MUNGU KABISA-KABISA, INAWEZA IKAKATALIWA NA WALIOOKOKA KABISA WENZAKO NA PIA WASIOOKOKA
LAKINI USIFE MOYO, USIPOE KATU KAMWE FIRE NDANI YAKO YA KUZIDI KUCHAPA KAZI YA BWANA, SIMAMA FIRM KABISA, PIGA KAZI YA MUNGU
SHIRIKISHA WANAOKUKUBALI, WAKUOMBEE NA UJIOMBEE MWENYEWE KWA BIDII KAMA MTUME PAULO, ALIVYOFANYA
Amani ya Bwana, iwe pamoja nanyi, enyi nyote, Amen.
Bwana Yesu mwenyewe kabisa-kabisa, mtume wake chuma kweli kweli cha kazi-Paulo, walikuwa na vitu vya Kimungu vizito sana. Waliitwa katika utumishi mkuu, walipewa huduma, missions na Mungu za ajabu- Luka. 4.18-20, 40-44, Luka. 19:10, Matendo. 9:1-22, Matendo. 22:1-21
Lakini ziko nyakati, walipokua wakichakalika kuchapa kazi ya Mungu, amini usiamini, walikataliwa. Walipingwa, walikosa kibali kwa watu ingawa walikua wamebeba toka kwa Mungu, mambo mazito kabisa yenye faida ya milele na milele kwa wanadamu
Ikiwa unapenda kujifunza Neno kwa kusoma maandiko, basi nimeweka ya kutosha. Ingawa ni kwa kuchagua baadhi ya mistari ili post isiwe ndefu kupita kiasi ila nimekuonyesha mistari yote unayotakiwa kujisomea.
Pia waweza kuongezea maandiko mengine uyajuayo ili kukazia ukweli huu wa maisha ya huduma, mwito na utumishi wa Bwana Yesu, mtume Paulo na sisi leo na vile mtume Paulo alifanya wakati alipokuwa hakubaliki kwa kile chema alichopewa na Bwana.
A: Matendo. 9: 1-22….. 20 Mara akamhubiri Yesu katika masinagogi, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu. 21 Na wote waliosikia wakashangaa, wakasema, Siye huyu aliyewaharibu walioliitia Jina hili huko Yerusalemu? Na hapa alikuwa amekuja kwa kusudi hilo, awafunge na kuwapeleka kwa wakuu wa makuhani?
26 Na Sauli alipofika Yerusalemu, alijaribu kujiunga na wanafunzi, nao walikuwa wakimwogopa wote, wasisadiki ya kuwa yeye ni mwanafunzi. 27 Lakini Barnaba akamtwaa, akampeleka kwa mitume, akawaeleza jinsi alivyomwona Bwana njiani, na ya kwamba alisema naye, na jinsi alivyohubiri kwa ushujaa katika Dameski kwa jina la Yesu.
28 Naye akawa pamoja nao katika Yerusalemu akiingia na kutoka. 29 Akahubiri kwa jina la Bwana kwa ushujaa, akinena na kuhojiana na Wayahudi wa Kiyunani. Nao wakajaribu kumwua.
===========
B: Matendo. 22: 3-30….. 7 Nikaanguka nchi, nikasikia sauti ikiniambia, Sauli, Sauli, mbona unaniudhi? 8 Nikajibu, Wewe u nani, Bwana? Akaniambia, Mimi ni Yesu Mnazareti, ambaye wewe unaniudhi. 9 Na wale waliokuwa pamoja nami waliiona ile nuru, lakini hawakuisikia ile sauti ya yule aliyesema nami.
10 Nikasema, Nifanye nini, Bwana? Bwana akaniambia, Simama, uingie Dameski, na huko utaambiwa habari za mambo yote yaliyoamriwa uyafanye. 11 Na nilipokuwa sioni kwa sababu ya fahari ya nuru ile, nikaongozwa na mikono yao waliokuwa pamoja nami, nikaingia Dameski.
12 Basi mtu mmoja, Anania, mtauwa kwa kuifuata sheria, aliyeshuhudiwa wema na Wayahudi wote waliokaa huko,13 Akanijia, akasimama karibu nami, akaniambia, Ndugu yangu Sauli, uone. Nikamwinulia macho yangu saa ile ile.
14 Akasema, Mungu wa baba zetu amekuchagua wewe upate kujua mapenzi yake, na kumwona yule Mwenye haki, na kuisikia sauti itokayo katika kinywa chake.
15 Kwa maana utakuwa shahidi wake kwa watu wote, wa mambo hayo uliyoyaona na kuyasikia. 16 Basi sasa, unakawilia nini? Simama, ubatizwe, ukaoshe dhambi zako, ukiliitia jina lake.
17 Ikawa nilipokwisha kurudi Yerusalemu, nilipokuwa nikisali ndani ya hekalu, nikawa hali ya kuzimia roho,18 nikamwona, naye akiniambia, Hima, utoke Yerusalemu upesi, kwa sababu hawatakubali ushuhuda wako katika habari zangu.
19 Nami nikasema, Bwana, wanajua hao ya kuwa mimi nalikuwa nikiwafunga gerezani wale wanaokuamini na kuwapiga katika kila sinagogi. 20 Na damu ya Stefano shahidi wako ilipomwagwa, mimi nami nilikuwa nikisimama karibu, nikikubali, na kuzitunza nguo zao waliomwua. 21 Naye akaniambia, Enenda zako; kwa kuwa mimi nitakutuma uende mbali kwa watu wa Mataifa
============
C: Warumi. 15: 14-33….. 19 kwa nguvu za ishara na maajabu, katika nguvu za Roho Mtakatifu; hata ikawa tangu Yerusalemu, na kando kando yake, mpaka Iliriko nimekwisha kuihubiri Injili ya Kristo kwa utimilifu, 20 kadhalika nikijitahidi kuihubiri Injili, nisihubiri hapo ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine;
30 Ndugu zangu, nawasihi kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa upendo wa Roho, jitahidini pamoja nami katika maombi yenu kwa ajili yangu mbele za Mungu 31 kwamba niokolewe na wale wasioamini katika Uyahudi, na tena huduma yangu niliyo nayo huko Yerusalemu ikubalike kwa watakatifu; 32 nipate kufika kwenu kwa furaha, kama apendavyo Mungu, nikapate kupumzika pamoja nanyi.
==============
D: Wagalatia. 2: 6 Lakini wale wenye sifa ya kuwa wana cheo; (walivyokuwa vyo vyote ni mamoja kwangu; Mungu hapokei uso wa mwanadamu); nasema, hao wenye sifa hawakuniongezea kitu;7 bali, kinyume cha hayo, walipoona ya kuwa nimekabidhiwa injili ya wasiotahiriwa, kama vile Petro ya waliotahiriwa;8 (maana yeye aliyemwezesha Petro kuwa mtume wa waliotahiriwa ndiye aliyeniwezesha mimi kwenda kwa Mataifa);
9 tena walipokwisha kuijua ile neema niliyopewa; Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;10 ila neno moja tu walitutakia, tuwakumbuke maskini; nami neno lilo hilo nalikuwa na bidii kulifanya.
Bwana Yesu kabisa-kabisa, kwa baadhi, alikataliwa, pingwa, kosa kibali na huduma yake
E: Matendo. 4: 1-14…. 8 Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia, Enyi wakubwa wa watu na wazee wa Israeli, 9 kama tukiulizwa leo habari ya jambo jema alilofanyiwa yule mtu dhaifu, jinsi alivyoponywa,
10 jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu.
11 Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni.12 Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
===============
F: Mathayo. 13: 53-58…. 54 Na alipofika nchi yake, akawafundisha katika sinagogi lao, hata wakashangaa, wakasema, Huyu amepata wapi hekima hii na miujiza hii?55 Huyu si mwana wa seremala? Mamaye si yeye aitwaye Mariamu? Na nduguze si Yakobo, na Yusufu, na Simoni, na Yuda?56 Na maumbu yake wote hawapo hapa petu? Basi huyu amepata wapi haya yote?
57 Wakachukizwa naye. Yesu akawaambia, Nabii hakosi kupata heshima, isipokuwa katika nchi yake, na nyumbani mwake mwenyewe. 58 Wala hakufanya miujiza mingi huko, kwa sababu ya kutokuamini kwao.
===============
G: Marko.6: 1-6…… 1 Akatoka huko, akafika mpaka nchi ya kwao; wanafunzi wake wakamfuata.2 Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake?
3 Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake.
4 Yesu akawaambia, Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake mwenyewe, na kwa jamaa zake, na nyumbani mwake. 6 Akastaajabu kwa sababu ya kutokuamini kwao. Akazunguka-zunguka katika vile vijiji, akifundisha.
HITIMISHO: Siyo kila huduma isiyokubalika na waliookoka wenzetu, ni shoti, imetoka kuzimu, ni ya Shetani. Ni kweli ziko huduma zinakataliwa kwakua chanzo chake ni wanadamu wajanja-janja tu, waliojipa huduma bila kuitwa na Mungu katika utumishi ili kuramba noti za wasiojua mambo ya Mungu, ya wokovu, maombi, maombezi, imani, mambo ya rohoni, ya kiroho, ya Neno na maandiko swadakta kabisa.
Habari njema ni kwamba, ikiwa ni kweli Mungu ndiye aliyekupa huduma, ni Bwana mwenyewe alikuita, ndiye alikupa hiyo kitu moyoni mwako basi, mwishowe ni kwamba, wewe na Bwana Yesu pia Mungu Baba, mtashinda na zaidi ya kushinda- Warumi.8: 37 Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.
Ukikaza kumtumikia na kufanya kazi yake, Mungu Baba atakuheshimu- Yoh. 12: 26 Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.
Na tena utatetewa na Bwana kiasi kwamba, zitakuja siku, hata waliokukataa, kupinga, wengine wataishilizia kukukubali sana mpaka kuwa watu wako muhimu sana kwa huduma hiyo hiyo walioisaga-saga.
Bwana Mungu, awabarikini, ninyi nyote, Eeiimen.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.