Mwachie Mungu asafishe jina lako.

Ninakukaribisha leo tena katika ujumbe huu mfupi wa Neno la Mungu,
Ujumbe ambao Roho Mtakatifu ameuachilia moyoni mwangu,
Nami nimeona si mbaya kama nikikushirikisha.

✍🏿Limekuwa hitaji la Watu waliosingiziwa, waliochafuliwa, kutaka yule aliyemchafua amsafishe mbele za watu.

Wengine wamekuwa wakidai hata pesa tena mamilioni ya pesa kama njia ya kurudisha thamani yao iliyochafuliwa.

✍🏿 Nimekuwa nikisoma Biblia kwa umakini sana ili nione ni wapi imeandikwa kuwa Yusufu aliomba pesa ili kusafisha jina lake mbele ya watu kwa yale aliyokuwa amesingiziwa na mke wa Potifa.

✍🏿 Zaidi sana sijaona ni wapi Farao alifanya kikao cha kumsafisha Yusufu mbele za watu kabla ya kumpa Uwaziri mkuu.

✍🏿 Isipokuwa namuona Farao akijawa na uso wa furaha akisema kwa sauti ya mamlaka, TUPATE WAPI MTU KAMA HUYU MWENYE ROHO WA MUNGU NDANI YAKE?

✍🏿 Ijapokuwa Yusufu alikuwa amesingiziwa,hata hivyo Yusufu akatolewa akawa juu hata ya wale waliomshtaki. MWANZO 39:41.

✍🏿 Mpendwa huenda wewe ni mmoja wa watu waliosingiziwa, wamekuzushia uongo,hata umejikuta thamani yako ikipotea mbele za watu,
Umejikuta thamani yako ikipotea hata mbele za mwenzi wako, mbele ya watoto wako, mbele za washirika wenzako.

✍🏿 Umehuzunika,umelia hadi machozi yamekauka,
Ukitembea unakuwa kama umechanganyikiwa kutokana na mawazo,
Wale walio kuwa marafiki zako wamekukimbia hawakuamini umekosa msaada.

🙏🏼 Leo nimetumwa kwako nikuambie UMWACHIE MUNGU AKUSAFISHE,
Mungu alisafishe jina lako lililochafuliwa na watu hata wale uliowaamini.

✍🏿 Mpendwa ukidai kusafishwa na wanadamu”UKOKO”utakubakia mwilini na moyoni.

✍🏿 Tena mwanadamu anaweza kukusafisha isivyo stahili,
✍🏿 Mwanadamu anaweza kukusafisha jinsi usitakate.

✍🏿 LAKINI ukisafishwa na Mungu,USAFI WAKO UTADUMU na utapata kibali hata mbele ya waliokuchukia na waliokushtaki.

✍🏿 Mpendwa mfuasi wa Yesu Kristo, Mungu ndiye anayeweza kuubeba unyonge wako na kuyakausha machozi yako.

HIVYO MWACHIE YEYE AKUSAFISHE.

KUMBUKA BAADA YA KUSAFISHWA NA MUNGU KUNA KUINULIWA

MPENDWA MUNGU AKIKUSAFISHIA JINA LAKO LILILO CHAFULIWA
HUWA ANALETA KUINULIWA KWAKO

NA UNAPOINULIWA NA MUNGU UTAMILIKI NA KUTAWALA HATA WALE WALIO KUWA MAADUI ZAKO.

Mwachie Mungu asafishe jina lako,wala siyo mwanadamu.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment