Usijidanganye pasipo na wewe mtu hawezi kufaulu

Kwenye maisha usije kujidanganya kuwa bila wewe mtu fulani hawezi kufanikiwa hata kama umefanyika msaada kwake na kuwa mtu wa muhimu kiasi gani. Dhana ya aina hiyo ni upumbavu wa kiwango cha juu. Unapaswa kutambua kuwa unapoondoka kwa kiburi kwenye maisha ya mtu, basi Mungu huwa anafungua mlango mwingine mkubwa zaidi yako wewe. Aliyetupatia mdomo ndiyo anaetupatia chakula na utukufu wake huwa hashirikiani na mtu yeyote. Ibrahimu alimwambia mfalme wa Sodoma kwamba, sitachukua hata uzi katika hivi vitu unavyonipa, ili Mungu atakaponibariki usije kusema kuwa ni wewe ndiyo ulinitajirisha. Tukiwa kama watu wa Mungu tunapaswa kuwaepuka sana watu wanaodhania kuwa ili Mungu atubariki ni lazima awatumie wao, na kwa kufanya hivyo tutakuwa tumetoa nafasi ya Mungu kuwaonyesha kuwa hata kama wao hawatamsifu bado ana uwezo wa kuyainua mawe na yakafanyika sifa za Mungu kwenye maisha yetu na tukalitukuza jina lake kupitia mawe hayo.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment