HUU MSTARI TUMEUKOSEA SANA KILICHOMAANISHWA NA MTUME PAULO, TUMEUPACHIKIA MENGINE KWA MUDA MREFU, TUREKEBISHENI,HATUJACHELEWA
Ukisoma huu mstari pekee yake bila kuzingatia mingine kabla na baada yake huu… ”Wafilipi. 4:13 Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu”’, ni rahisi kuupachikia maana nyingine ambayo siyo ile msemaji alimaanisha
Nafahamu kwamba, hakuna anayezaliwa kimwili na kisha kiroho- kuokoka, akajua yote bali tunakuwa wote katika safari ndefu sana ya kujifunza kila leo
Hata mie sikuwa naelewa lakini nimejifunza na kufunza mambo kadhaa na nimeendelea kuwa bora ingawa bado safari ya kujifunza inasonga mbele mpaka ajapo mwana wa Adamu.
Hapana kabisa kuona haya kwamba haujui maana kwa habari ya mambo ya Mungu,kiroho,rohoni, kila mtu alikua hajui na hata sasa kila mtu hajui yote bali anafahamu kwa sehemu-
1Wakorinto. 12:9 Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu;10 lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika.
11 Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto.
12 Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana.
Moja ya niliyojifunza ni kwamba, ni vizuri tunaposoma maandiko, tuzingatie kimtiririko wake, kwa muktadha wake. Kwa andiko hilo la Wafil. 4:13, hapo mtume Paulo alikua anamaanisha tu katika hali ya kuwanavyo au kukosa, anaweza mambo yote ktk Bwana.
Lisome sasa mwenyewe mistari yake kadhaa kabla na baada ya huo wa 13, utaelewa tu sana mbona tena swafi kabisa na rahisi sana
Wafilipi. 4: 8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.
9 Mambo mliyojifunza kwangu na kuyapokea, na kuyasikia na kuyaona kwangu, yatendeni hayo; na Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.10 Nalifurahi sana katika Bwana, kwa kuwa sasa mwisho mmehuisha tena fikira zenu kwa ajili yangu, kama vile mlivyokuwa mkinifikiri hali yangu lakini hamkupata nafasi.
11 Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo nayo.12 Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa.13 Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.
14 Lakini mlifanya vema, mliposhiriki nami katika dhiki yangu. 15 Nanyi pia, ninyi wenyewe mnajua, enyi Wafilipi, ya kuwa katika mwanzo wa Injili, nilipotoka Makedonia, hakuna kanisa lingine lililoshirikiana nami katika habari hii ya kutoa na kupokea, ila ninyi peke yenu.
16 Kwa kuwa hata huko Thesalonike mliniletea msaada kwa mahitaji yangu, wala si mara moja.17 Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu.
18 Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu.19 Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.
Mwenyezi Mungu atubarikie sisi sote, Amen
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.