Ukraine yasema uchaguzi utafanyika baada ya dhamana

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Ukrainian Presidential Office/AFP

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema nchi hiyo itafanya uchaguzi baada ya kupata dhamana za kiusalama na kufikiwa kwa usitishati mapigano na Urusi.

Kiongozi huyo amekanusha madai kwamba anapanga kuitisha uchaguzi mpya kufuatia shinikizo kutoka Marekani.

Gazeti la The Financial Times liliripoti kwamba Ukraine ilikuwa inafikiria uwezekano wa kufanya uchaguzi wa rais ndani ya miezi mitatu ijayo, ikidaiwa hali hiyo imetokana na shinikizo kutoka Washington.

Ripoti hiyo iliongeza kuwa tangazo la uchaguzi huenda lingetolewa tarehe 24 Februari, siku ambayo Ukraine inaadhimisha miaka minne tangu Urusi ilipoivamia kijeshi.

Hata hivyo, Zelensky amekanusha vikali taarifa hizo kupitia mtandao wa kijamii wa X, akisema kuwa kutumia tarehe hiyo kuzungumzia siasa ni “wazo la kipuuzi kabisa.”

Tangu Urusi ilipoivamia Ukraine mwaka 2022, nchi hiyo imekuwa chini ya sheria ya kijeshi na kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo, uchaguzi hauwezi kufanyika katika mazingira ya sasa.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply