Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Sir Keir Starmer ametaja maoni kuhusu uhamiaji yaliyotolewa na mmiliki mwenza na bilionea wa Manchester United Sir Jim Ratcliffe kuwa “ya kukera na yasiyo sahihi”.
Sir Jim, mwanzilishi wa kampuni kubwa ya kemikali duniani, Ineos, aliiambia Sky News Jumatano kwamba Uingereza ilikuwa “imetawaliwa na wahamiaji” na kusema waziri mkuu “ni mzuri sana” kufanya “mambo magumu” kuleta utulivu wa uchumi wa nchi.
Katika karipio lake Jumatano jioni, Sir Keir aliongeza kuwa Uingereza ni “nchi yenye fahari, vumilivu na yenye watu mbalimbali” na kumtaka Sir Jim kuomba radhi.
Msemaji wa afisi ya waziri mkuu pia alimtaka mfanyabiashara huyo kuomba radhi, akisema maoni “yanapendelewa na wale wanaotaka kugawanya nchi yetu”.
BBC imewasiliana na Ineos na Manchester United ili kutoa maoni yao kuhusiana na matamshi ya Sir Jim. Sir Jim aliliambia shirika la utangazaji:
“Huwezi kuwa na uchumi wenye watu milioni tisa wanaonufaika na viwango vikubwa vya wahamiaji wanaoingia.” Aliongeza: “Namaanisha, Uingereza imetawaliwa.
Inagharimu pesa nyingi sana. “Uingereza imetawaliwa na wahamiaji, sivyo? Ninamaanisha, idadi ya watu nchini Uingereza ilikuwa milioni 58 mnamo 2020, sasa ni milioni 70.
Hiyo ni watu milioni 12.” Hathivyo, data kutoka Ofisi ya Takwimu ya Kitaifa inakadiria kuwa idadi ya watu wa Uingereza katikati ya 2025 ilikuwa milioni 69.4, ikilinganishwa na milioni 66.7 katikati ya 2020.
Sir Jim alitoa maoni hayo wakati wa mahojiano na mhariri wa uchumi wa Sky News Ed Conway, pembezoni mwa Mkutano wa Kiwanda wa Ulaya huko Antwerp, Ubelgiji.
Matamshi hayo pia yalilaaniwa na makundi mbalimbali ya mashabiki, ikiwa ni pamoja na Manchester United Supporters Trust ambayo ilisema kwenye X: “Hakuna shabiki anayepaswa kuhisi kutengwa kuifuata au kuiunga mkono klabu kwa sababu ya rangi, dini, utaifa au asili yake.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.