Rais Samia Suluhu Hassan afikisha siku 100 madarakani.

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Rais Samia Suluhu Hassan anatimiza siku 100 tangu alipoapishwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaPicha: Tanzania State House

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefikisha siku 100 tangu aliporejea madarakani Novemba 5, 2025, huku Serikali ikimsifu kwa kutekeleza mambo mengi ya kimaendeleo.

Serikali imesema katika siku 100 za Rais Samia, ametekeleza mambo lukuki ikiwamo kukamilika kwa bima ya afya kwa wote, kuundwa kwa tume ya kuchunguza vurugu za Oktoba 29 na kutoa fedha za mikopo kwa vijana, hata hivyo inaelezwa suala la maridhiano ya kisiasa hasa baada ya vurugu za Oktoba 29 lina walakini. 

Siku 100 za kishindo lakini zenye maswali. Ndivyo baadhi wanavyosema wakati rais Samia Suluhu Hassan anapotimiza siku 100 tangu aapishwe rasmi kuwa Rais.

Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa amesema, Rais Samia ametimiza karibu ahadi zote alizotoa wakati wa kampeni, katika kipindi hiki cha miezi mitatu na siku 10.

Msemaji wa serikali ya Tanzania Gerson Msigwa amezungumzia siku 100 za Rais Samia Suluhu Hassan madarakani kwa kusema amefanikiwa pakubwa kutekeleza ahadi zake za wakati wa kampeniPicha: Privat

Aliongeza “Bima ya afya kwa wote kwa awamu imeanza, makundi yameanza kusajiliwa, lakini pia ameahidi katika siku 100 kuondoa jambo lililokuwa linawakera watu wengi la maiti kuzuiliwa pale ambapo wenye marehemu wamekosa fedha za matibabu”

Maswali yangalipo katika siku 100 za Samia

Ombwe kubwa katika siku 100 za Rais huyu wa kwanza mwanamke kwa Tanzania lilijitokeza baada ya vurugu za Oktoba 29 ambapo maswali ya wengi yalikuwa ni  taifa litaponaje ilhali watanzania walio wengi wana makovu. Msigwa anaeleza.

Msigwa alisema “Utakubaliana nami hakuna mtanzania aliyetegemea yaliyotokea Oktoba 29 kwa hiyo busara ikaongoza kwamba yale yaliyotokea 29 na siku kadhaa kabla yatolewe majawabu kwanza kabla ya kuendelea na mchakato wa maridhiano.”

Rais Samia Suluhu Hassan anafikisha siku 100 madarakani, katikati ya mchakato wa maridhiano kufuatia vurugu za uchaguzi wa Oktoba 29, 2025Picha: AFP

Ahadi za Rais Samia zimeanza kutimizwa

Katika uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2025, Rais Samia Suluhu Hassan aliweka wazi dira yake  katika siku 100 za mwanzo na kusema analenga kugusa maisha ya watu ikiwamo katika sekta nyeti za afya na elimu.

Rais Samia aliahidi kuajiri watumishi 12,000 ili kuimarisha utoaji wa huduma katika sekta hizo mbili, kuanza majaribio ya mpango wa bima ya afya kwa wote kama hatua kuelekea huduma jumuishi za afya.

Kadhalika alisisitiza  hospitali hazitaruhusiwa tena kuzuia miili ya marehemu kwa kisingizio cha madeni ya matibabu.

Wafuatiliaji watoa wito wa subira

Tanzania: Ushahidi mpya juu ya mauaji ya Oktoba 2025

Mchambuzi wa masuala ya diplomasia na siasa wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Dk Revocatus Kabobe, anasema ni mapema kumuhukumu Rais Samia katika siku 100 hasa linapokuja suala la makovu ya Oktoba 29

“Mimi nadhani siku hizi 100 kuzitumia kutoa hukumu au kufanya tathmini ya yaliyotokea Oktoba 29 nadhani tusubirie tume, majibu ya tume, nini wamegundua, wameona nini, chanzo cha vurugu kilikuwa ni nini tunatokaje hapatunatokaje hapa, tume ikishatoa ripoti yake, na mimi natamani ripoti hiyo iwe hadharani,” alisema Kabobe.

Wachambuzi na wanazuoni wanazitathmini siku 100 za Rais Samia wakilinganisha na muhula wake wa kwanza alipopokea kijiti kutoka kwa hayati John Pombe Magufuli, wakisema siku 100 za wakati ule zilikuwa zaidi katika kuendeleza aliyoyafanya mtangulizi wake lakini siku 100 za sasa zinamuhitaji Rais Samia  kuwekeza katika maridhiano

Pamoja na mambo mengine Rais Samia katika siku zake 100 mara kadhaa amefanya mabadiliko katika baraza la mawaziri mara kadhaa akitaja sababu kuwa ni kuongeza uwajibikaji, kasi ya utekelezaji na kuongeza ufanisi serikalini.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment