Ghana yatangaza Jumatano kuwa ‘Siku ya kuvaa Fugu’ vazi la kitamaduni baada ya kejeli mtandaoni

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

.

Ghana imetenga kila Jumatano kama siku ya kuvaa vazi la kitamaduni la nchi hiyo, fugu, siku chache baada ya kuzua mjadala mtandaoni na Wazambia.

Vazi hilo lilipata umaarufu wiki iliyopita wakati Rais John Dramani Mahama alipolivaa wakati wa ziara ya kitaifa nchini Zambia, ambapo baadhi waliliita kwa kejeli “blauzi,” na kusababisha mwitikio mkali kutoka kwa Waghana mtandaoni.

Waziri wa Utalii wa Ghana Abla Dzifa Gomashie alisema Jumanne kwamba kuvaa vazi hilo kila wiki kutasaidia kuonyesha utambulisho wa nchi hiyo “kwa fahari katika jukwaa la kimataifa”.

Alihimiza kuvaa vazi hilo “aina zake zote, miundo, na mishono yake mbalimbali, likiongezewa na nakshi zake zake za kipekee zenye kuvutia”.

Fugu, ambayo pia inajulikana kama batakari, ni nguo ya kitamaduni inayovaliwa seheme ya juu ya mwili kutoka kaskazini mwa Ghana iliyotengenezwa kwa vipande vyembamba vya kitambaa kinene cha pamba vilivyoshonwa pamoja ili kuunda vazi lenye muundo wa mtindo wa poncho.

Zaidi ya umuhimu wake wa kitamaduni, Gomashie alisema maonyesho ya kila wiki ya mavazi hayo “yataleta faida kubwa za kijamii na kiuchumi” hasa kwa wafumaji, wabunifu, mafundi na wafanyabiashara wa ndani.

“Serikali inatumai kwamba mtindo wa kuvaa Fugu kutaimarisha umoja wa kitaifa, kuchochea uchumi wa ubunifu, na kutumika kama ishara yenye nguvu ya kujiamini kitamaduni na kujieleza Kighana,” waziri huyo aliongeza.

Mavazi hayo yamekuwa maarufu kwenye mitandao ya kijamii kwa siku kadhaa kufuatia utani kati ya Waghana na Wazambia.

Mjadala huo uliwafanya Waghana, wakiwemo wabunge, kufurika kwenye mitandao ya kijamii wakionyesha kwa fahari nguo zao aina ya fugu, huku Wazambia wakionekana wakiwa wamevaa mavazi yao ya kitamaduni yanayojulikana kama siziba.

Mazungumzo hayo ya mtandaoni yalivutia nadhari ya Rais wa Zambia Hakainde Hichilema, ambaye alitangaza kwamba nchi yake ingeagiza nguo za fugus kutoka Ghana.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment