Netanyahu kufanya mazungumzo na Trump Washington

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais Donald Trump wa MarekaniPicha: Jonathan Ernst/REUTERS

Rais wa Marekani Donald Trump atakuwa mwenyeji wa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu leo.

Kulingana na Netanyahu, mazungumzo yake na Trump katika ikulu ya White House yatajikita katika mazungumzo ya Marekani na Iran.

Waziri mkuu huyo wa Israel amesema atauwasilisha mtazamo wa Israel katika mazungumzo hayo na Jamhuri hiiyo ya Kiislamu.

Viongozi hao wawili pia wataijadili hali katika Ukanda wa Gaza na eneo zima la Mashariki ya Kati.

Gazeti moja la Israel limeripoti kuwa Netanyahu anapania kumpa Trump taarifa za kiintelijensia kuhusu mpango wa makombora wa Iran, pamoja na mauaji ambayo Iran imeyafanya dhidi ya raia wake, wakati wa maandamano ya wiki chache zilizopita ya kuipinga serikali.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment