Iran yaadhimisha miaka 47 ya Mapinduzi ya Kiislamu

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph/RFA/ AP/AFP/RTRE/DPA

Wairan wamekusanyika mjini Tehran, karibu na Mnara wa Azadi wakati wa maadhimisho ya miaka 47 ya Mapinduzi ya KiislamuPicha: Majid Asgaripour/WANA/REUTERS

Iran yaadhimisha miaka 47 ya Mapinduzi ya Kiislamu huku utawala wa nchi hiyo ukiendelea kukabiliwa na shinikizo kutoka kwa raia wake na Marekani inayojiandaa kupeleka meli nyingine ya kivita Mashariki ya Kati.

Katikati mwenye shati Jeupe: Rais wa Iran Masoud Pezeshkian kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya Mapinduzi ya KiislamuPicha: Iranian Presidency/ZUMA/picture alliance

Pande mbili za Wairan wanaoiunga serikali na wale wanaopinga utawala wa Iran zimejitokeza barabarani kuadhimisha miaka 47 ya Mapinduzi ya Kiislamu yaliyofanyika mwaka 1979.

Katika hotuba yake Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Masoud Pezeshkian, ameomba radhi kwa wote walioathiriwa wakati wa maandamano ya kitaifa yaliyosababisha umwagikaji damu ambapo amelaumu kile alichokiita “propaganda za Magharibi” zinazohusishwa na maandamano hayo.

Utawala wa Iran unakabiliwa na shinikizo kutoka kwa raia wake wanaopinga na kulaani nguvu zilizotumiwa na maafisa wa usalama nchini mwao dhidi ya waandamanaji na wakati huo huo Rais wa Marekani Donald Trump amependekeza kupeleka meli nyingine ya kivita katika eneo la Mashariki ya Kati.

Rais wa Iran katika hotuba yake amesisitiza kwamba taifa lake halitafuti kuunda silaha za nyuklia na kwamba liko tayari kuthibitisha hilo kwa njia yoyote ile. Hata hivyo, uongozi wa Iran bado una mashaka kuhusu mazungumzo na adui yake mkuu, Marekani.

Kushoto: Sultan wa Oman Haitham bin Tariq. Kulia: Mkuu wa maswala ya Usalama wa Iran Ali LarijaniPicha: Iranian Security Council Press Office/Anadolu/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amesema nchi yake bado “haina imani kamili na Wamarekani.” Licha ya wasiwasi uliopo, Araghchi amesema inawezekana wakati huu Iran na Marekani zikafikia makubaliano bora zaidi ya nyuklia kuliko ya wakati wa Rais Barack Obama ya mwaka 2015 na mataifa yenye nguvu duniani ambayo Trump katika muhula wake wa kwanza aliiondoa Marekani kutoka kwenye makubaliano hayo.

Wakati huo huo afisa mkuu wa maswala ya usalama wa Iran Ali Larijani anaeleka Qatar hii leo Jumatano baada ya safari yake huko Oman, nchi ambayo ndiyo iliongoza duru ya hivi karibuni ya mazungumzo kati ya Iran na Marekani.

Na Emir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani amejadiliana kwa njia ya simu na Rais wa Marekani Donald Trump, katika juhudi za kupunguza vitisho vya usalama na kuhakikisha utulivu katika kanda ya Mashariki ya Kati.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment