Marekani yatuma wanajeshi 200 Nigeria

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Wanajeshi wa MarekaniPicha: Daniel Karmann/dpa/picture alliance

Vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kwamba kupelekwa kwa wanajeshi hao kutaongeza idadi ya timu ndogo ambayo tayari iko nchini Nigeria ili kusaidia katika kutoa mafunzo,mwongozo wa kiufundi na kufanya mashambulizi.

Kamandi ya jeshi la Marekani ya Afrika imesema kwamba Marekani itapeleka wanajeshi 200 nchini Nigeria kutoa mafunzo kwa jeshi la nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika katika mapambano yake dhidi ya makundi ya kigaidi.

Vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kwamba kupelekwa kwa wanajeshi hao kutaongeza idadi ya timu ndogo ambayo tayari iko nchini Nigeria ili kusaidia katika kutoa mafunzo,mwongozo wa kiufundi na kufanya mashambulizi.

Utawala wa Trump umekuwa ukisisitiza kuwepo kwa matukio ya kulengwa na kuuliwa kwa Wakristo nchini Nigeria ingawa Nigeria yenyewe imekuwa ikakanusha madai hayo na kusema kwamba jamii zote mbili za waikristo na waislamu ni wahanga wa matukio hayo ya  kigaidi.

Kwa miaka mingi Nigeria imekuwa ikipambana na makundi ya kijihadi kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ambayo yamekuwa yakiua, yakiteka nyara, kupora na kudai fidia.
 

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment