Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Umoja wa Mataifa umeonya juu ya kuibuka kwa janga kubwa kabisa la kibinaadamu katika mkoa wa Kordofan huko El Fasher, ambako wakazi kama walioko pichani walikimbia mapigano kwenye eneo hiloPicha: Ebrahim Hamid/AFP
Mkuu wa Shirika la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa limesema ukatili uliofanywa kwenye mji wa El-Fasher nchini Sudan ulikuwa ni “janga la haki za binadamu ambalo lingeweza kuzuilika.”
Mkuu wa Shirika la Haki za Binaadamu ametahadharisha juu ya hatari ya janga hilo kujirudia kwenye eneo jirani la Kordofan.
Akitoa taarifa mpya kwa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja huo kuhusu hali huko El-Fasher Volker Turk alilaani matukio ya kutisha baada ya wanamgambo wa RSF kuanzisha “wimbi la vurugu”, wakati ilipouzingira kwa miezi 18, mwezi Oktoba mwaka uliopita.
Amesema “Tulisikia ushuhuda kwamba baadhi ya waathiriwa walilengwa kwa misingi ya kikabila, ambalo sio la Kiarabu – haswa, watu wa kabila la Zaghawa. Manusura pia walituambia walishuhudia marundo ya maiti kando ya barabara zinazoelekea El Fasher na kwingineko, katika tukio lililokuwa la kutisha mno ambalo, shuhuda mmoja alilifananisha na Siku ya Hukumu.”
Ametahadharisha ni dhahiri kutatokea janga kubwa zaidi ikiwa ulimwengu utaendelea kutizama pande zinazopigana zikiendelea kutenda uhalifu wa wazi, huku akionyesha wasiwasi kwamba ukiukwaji na unyanyasaji huo unaweza kurudiwa katika eneo la Kordofan.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.