Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA
Iran imeonya leo Jumanne kuhusu ushawishi wa Israel utakaovuruga mchakato wa diplomasia kabla ya ziara ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu huko Washington.

Iran imeonya kuhusu ushawishi wa Israel utakaovuruga mchakato wa diplomasia unaoendelea kati ya Iran na MarekaniPicha: Foad Ashtari/SOPA Images/IMAGO
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Esmail Baqaei amewaambia waandishi wa habari kwamba Marekani ndio mshirika wao kwenye mazungumzo ya nyuklia na ni jukumu lake kufanya maamuzi nje ya mashinikizo ama ushawishi utakaoivuruga kanda hiyo.
Amesema utawala wa Kizayuni umeonyesha mara kwa mara kuhujumu na kupinga mchakato wowote wa kidiplomasia utakaopelekea amani katika eneo lao.
Netanyahu atafanya mazungumzo na Rais Donald Trump yanayotarajiwa kujikita kwenye mchakato unaoendelea wa makubaliano kati ya mataifa hayo mawili kuhusu silaha za nyuklia za Iran ulioanza tena Ijumaa iliyopita huko Muscat.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.