Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA
Mkuu wa Operesheni za kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani Pierre Lacroix, ameanza ziara ya siku tatu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Katika ziara hiyo, Umoja wa Mataifa unasema, Lacroix, atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbali wa kisiasa, mashirika ya kiraia na viongozi wa dini, kuthathmini hali ya amani hasa Mashariki mwa nchi hiyo.
Ziara yake inakuja, katika kipindi ambacho Umoja wa Mataifa unatarajiwa kutuma waangalizi wake huko Uvira, kuthathmini mwenendo wa utekelezwaji wa mkataba wa amani, baada ya waasi wa M23/AFC kuondoka katika mji huo waliokuwa wameutaka.
Mbali na jukumu la kulinda amani na raia, kikosi cha MONUSCO kwa mujibu wa azimio la Baraza la Usalama namba 2808 la mwaka 2025, jukumu lake pia ni kuhakikisha inaunga mkono utekelezwaji wa mkataba wa kusitisha vita.
Aidha, ziara yake inakuja wakati huu Afrika Kusini ikiangaza mwishoni mwa wiki iliyopita, kuwa itaondoa wanajeshi wake 700 wanaounda kikosi cha MONUSCO, kufikia mwisho wa mwaka huu, baada ya jitihada za nchi hiyo kuunga mkono upatikanaji wa amani nchini DRC kwa miaka 27.
Mwaka 2025, Afrika Kusini pia iliondoa wanajeshi wake, katika kikosi cha SADC baada ya kuuawa kwa wanajeshi wake 17 katika mzozo kati ya waasi wa M23/AFC na vikosi vya Jumuiya hiyo ya Kusini mwa Afrika.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.