Wanajeshi wa Libya wasambaza mafuta kwa kikosi cha RSF nchini Sudan – The Sentry

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

.

Kikundi cha uratibu chenye makao yake Marekani kinasema kwamba wanajeshi wanaomuunga mkono kamanda wa Libya, Khalifa Haftar, wamekuwa wakisambaza mafuta kwa Kikosi cha Rapid Support Forces (RSF) nchini Sudan kwa niaba ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Kundi hilo, lijulikanalo kama The Sentry, linasema Haftar amekuwa msambazaji muhimu wa mafuta na silaha kwa RSF wakati wote wa vita.

Kamanda huyo wa Libya ameshtumiwa mara si moja kwa kusambaza silaha na mafuta kwa kikosi cha RSF kwa niaba ya falme za kiarabu, madai ambayo amekanusha.

Falme za kiarabu pia imekanusha kuhusika na vita vinavyoendelea Sudan.

Ripoti ya The Sentry inasema kuwa, hatua ya Haftar kuwapa mafuta kikosi cha RSF, kumewasaidia kudhibiti eneo la Darfur ambayo sasa ni ngome yao kuu.

Eneo zima la Darfur magharibi mwa Sudan, linapakana na Libya pamoja na Chad, na liko chini ya udhibiti wa RSF ambao waliuteka mji wa mwisho wa El-Fasher ambao ulikuwa unadhibitiwa na jeshi la Sudan.

Ripoti ya Umoja wa mataifa, imeishtumu falme za kiarabu kwa kuipa RSF silaha na ndege za kivita zisizo na rubani.

Jeshi la Sudan, pia limeshtumu Falme za Kiarabu kwa kuwatuma mamluki kutoka Colombia kupitia mataifa jirani kupigana vita vinavyoendelea nchini humo.

Mshauri wa Rais wa Falme za Kiarabu (UAE), Anwar Gargash, alilaani ukatili unaoendelea mjini El-Fasher na kupinga vikali kile alichokiita “habari za uongo” kuhusu Falme za Kiarabu kuhusika na vita vinavyoendelea Sudan.

Libya imegawanyika kati ya serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa mjini Tripoli, inayoongozwa na Waziri Mkuu Abdulhamid Dbeibah, na utawala wa Haftar ulioko mashariki mwa nchi hiyo.

Taifa hilo la kaskazini mwa Afrika, limegawanyika tangu mapinduzi yaliyotokea mwaka wa 2011, yaliyomuondoa madarakani kiongozi wa muda mrefu wa taifa hilo Muammar Gaddafi.

Kiongozi wa zamani Bangladesh ameiambia BBC kuwa hana hatia ya uhalifu dhidi ya binadamu

.

Waziri mkuu wa zamani wa Bangladesh Sheikh Hasina amekanusha kutenda uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa msako mkali dhidi ya maasi ya mwaka jana yaliyomuondoa madarakani, siku chache kabla ya mahakama maalum inayomkabili kutoa uamuzi.

Hasina anatuhumiwa kuwa nyuma ya mamia ya mauaji wakati wa maandamano makubwa ya kupinga utawala wake wa kiimla – madai ambayo anayakanusha.

Katika mahojiano yake ya kwanza na BBC tangu atoroke nchini tarehe 5 Agosti 2024, alisema kesi yake bila kuwepo mahakamani ilikuwa “ujinga” uliopangwa na “mahakama isiyo na haki” inayodhibitiwa na wapinzani wa kisiasa.

Waendesha mashtaka wanatafuta hukumu ya kifo kwa Hasina iwapo atapatikana na hatia siku ya Jumatatu.

Israel yapokea maiti huku Hamas ikisema ni ya mateka

.

Israel imethibitisha kuwa imepokea jeneza ambalo Hamas inasema lina mwili wa mateka mwingine.

Magari ya Shirika la Msalaba Mwekundu yalichukua mwili huo saa chache baada ya Hamas kutoa taarifa ya pamoja na Palestina Islamic Jihad ikisema imeipata katika eneo la Khan Younis kusini mwa Gaza.

Ofisi ya waziri mkuu wa Israel ilisema mwili huo utahamishiwa Israel, ambapo utapokelewa katika sherehe za kijeshi kabla ya kufanyiwa mchakato wa utambulisho.

Kuthibitishwa kuwa ni maiti ya mateka kutamaanisha kuwa mateka 25 kati ya 28 waliofariki wamekabidhiwa kwa Israel chini ya awamu ya kwanza ya makubaliano ya sasa ya kusitisha mapigano ambayo ni sehemu ya mpango wa Marekani wa kumaliza vita vya Gaza.

BBC yamwomba Trump msamaha lakini imekataa kulipa fidia

.

BBC imemuomba msamaha Rais wa Marekani Donald Trump kwa kipindi cha Panorama ambacho kiliunganisha sehemu za hotuba yake ya tarehe 6 Januari 2021, lakini ikakataa madai yake ya kulipwa fidia.

Shirika hilo lilisema hariri hiyo imetoa “hisia potofu kwamba Rais Trump alikuwa ametoa mwito wa moja kwa moja wa vitendo vya vurugu” na kusema kwamba haitaonyesha mpango wa kipindi hicho wa mwaka 2024 tena.

Mawakili wa Trump wametishia kuishtaki BBC kwa fidia ya $1bn (£759m) isipokuwa shirika hilo liondoe makala hiyo, liombe msamaha na kumfidia.

Kutokea kwa kashfa hiyo kulisababisha mkurugenzi mkuu wa BBC Tim Davie na mkuu wa habari Deborah Turness kujiuzulu siku ya Jumapili.

“Tunakubali kwamba hariri yetu bila kukusudia ilisababisha hisia kwamba tulikuwa tukionyesha sehemu moja ya hotuba inayoendelea, badala ya nukuu kutoka kwa vidokezo tofauti kwenye hotuba, na kwamba hii ilitoa maoni potofu kwamba Rais Trump alikuwa ametoa mwito wa moja kwa moja wa vitendo vya vurugu,” ilisema.

Mawakili wa BBC wameandikia timu ya wanasheria wa Rais Trump kujibu barua iliyopokelewa siku ya Jumapili, msemaji wa BBC alisema.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment