Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Wapalestina wa Al-Faraa wamesimama nje ya msikiti ulioharibiwa kufuatia shambulizi la jeshi la Israel, Magharibi ya Al-Faraa.Picha: Nasser Nasser/AP/picture alliance
Wizara ya Mambo ya Nje ya Mamlaka ya Palestina yenye makao yake Ramallah imesema kuwa walowezi wa Israel wameteketeza moto msikiti wa Hajja Hamida ulioko karibu na mji wa Deir Istiya, kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi.
Katika taarifa yake, wizara hiyo imeeleza kuwa tukio hilo linakiuka wazi utakatifu wa maeneo ya ibada na linaakisi ubaguzi uliokita mizizi unaowaongoza walowezi chini ya ulinzi wa serikali waliyoiita ya uvamizi.
Picha za shirika la habari la AFP zimeonyesha nakala za kitabu kitakatifu cha Quran zilizochomwa na kuta za msikiti zilichorwa kwa maandishi ya chuki.
Jeshi la Israel (IDF) limesema kuwa vikosi vya usalama vilitumwa katika eneo hilo baada ya kupokea taarifa kuhusu washukiwa walioteketeza msikiti huo kwa moto, lakini hakuna mtu yeyote aliyekamatwa.
Uchunguzi wa tukio hilo umehamishiwa kwa polisi wa Israel na taasisi za usalama.
IDF imelaani tukio hilo na kusisitiza kuwa itaendelea kufanya kazi ili kuhakikisha usalama na utulivu katika eneo hilo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, pia amelaani shambulio hilo kupitia msemaji wake, akieleza “Matendo ya vurugu yanayolenga maeneo ya ibada kamwe hayakubaliki.”
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.