Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na:Cantona Joseph|RFA

Droni ya Urusi mjini KyivPicha: Sergei Supinsky/AFP
Jeshi la Urusi limefanya mashambulizi makubwa mapema leo kwa kutumia droni na makombora yaliyoulenga mji mkuu wa Ukraine, Kyiv.
Maafisa wa Ukraine wamesema mashambulizi hayo yalilenga majengo mbalimbali na kusababisha milipuko na moto katika maeneo kadhaa ya mji huo.
Meya wa Kyiv, Vitali Klitschko, amethibitisha kuwa watu wawili wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo.
Kupitia ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa Telegram, meya huyo ameeleza kuwa mji wa Kyiv uko chini ya mashambulizi ya Urusi na akawahimiza wakaazi kutafuta maeneo salama ya kujihifadhi.
Mkuu wa utawala wa kijeshi wa Kyiv, Tymur Tkachenko, ametoa agizo kwa vikosi vya dharura kutumwa haraka katika maeneo yaliyoathirika ili kushughulikia athari za mashambulizi hayo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.