Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na :Cantona Joseph|RFA

Rais wa Israel Isaac Herzog amepokea barua kutoka kwa Rais wa Marekani Donald Trump ikimtaka rasmi “kumsamehe kikamilifu” Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.
Netanyahu amekuwa na kesi kwa miaka mitano iliyopita ya tuhuma za hongo, ulaghai na uvunjaji wa uaminifu kuhusiana na kesi tatu tofauti. Hata hivyo amekanusha kosa lolote.
Katika barua hiyo, Trump anaandika kwamba “kabisa” anaheshimu uhuru wa mfumo wa haki wa Israel, lakini anaamini kuwa Netanyahu anakabiliwa na “mashitaka ya kisiasa, yasiyo ya haki”.
Ofisi ya Herzog ilisema inampa Trump “heshima ya juu”, lakini kwamba yeyote anayetaka kusamehewa analazimika kuwasilisha ombi rasmi.
Netanyahu baadaye alimshukuru Trump kwa “msaada wake wa kipekee”.
“Kama kawaida, unaelewa kabisa na kachukua hatua bila pinda,” aliandika kwenye X. “Ninatarajia kuendeleza ushirikiano wetu ili kuimarisha usalama na kupanua amani.”
Mnamo mwaka 2020, Netanyahu alikua waziri mkuu wa kwanza wa Israel kufungulia kesi.
Katika kesi ya kwanza, waendesha mashitaka wamedai kwamba alipokea zawadi – hasa sigara na chupa za shampeni – kutoka kwa wafanyabiashara wa hadhi ya juu kwa mabadilishano ya kupata upendeleo.
Katika kesi ya pili, anashtakiwa kwa kujitolea kusaidia kuboresha usambazaji wa gazeti la Israeli kwa mabadilishano ya kuangaziwa kwa mtazamo chanya.
Trump atia saini mswada wa kumaliza mkwamo wa shughuli za serikali

Rais Donald Trump wa Marekani ametia saini mswada wa ufadhili wa kufungua tena shughuli za serikali ya Marekani na kumaliza mkwamo ambao umeshuhudiwa kwa muda mrefu zaidi katika historia ya nchi hiyo.
“Nchi haijawahi kuwa katika hali nzuri kama hii,” rais anasema kabla tu ya kutia saini mswada huo.
“Ni siku njema,” Trump aliendelea kusema wakati waandishi wa habari wanatolewa nje ya Ikulu.
Mswada huo utarejesha wafanyikazi wa serikali kazini, kutoa pesa kwa mashirika ya serikali, programu na idara na kurejesha malipo kwa mamia ya maelfu ya wafanyikazi ambao hawajalipwa tangu kuanza kwa mkwamo huo tarehe 1 Oktoba.
Kusimamishwa kwa shughuli za serikali kumeendelea kwa siku 43, ikipita rekodi ya hapo awali ya siku 35 – ambayo ilitokea wakati wa muhula wa kwanza wa Trump.
Wanandoa wa Uingereza walioshikiliwa Iran wasusia kula, amesema mtoto

Wanandoa wa Uingereza waliofungwa jela nchini Iran baada ya kushutumiwa kwa ujasusi wamesusia kula katika “kilio cha kuomba msaada”, mtoto wao ameiambia BBC.
Craig na Lindsay Foreman walikuwa katika safari ya pikipiki ya kuzunguka dunia walipokamatwa na mamlaka ya Iran mnamo mwezi Januari.
Joe Bennett, mtoto wa kiume wa Lindsay, alielezea mashtaka dhidi yao kama “upuuzi”. Alisema mama yake alimwambia “kutokula ndio nguvu pekee aliyonayo”, katika simu ya dakika saba na nusu ambayo aliruhusiwa Jumanne.
“Alisema alihisi kupotea na kukatishwa tamaa na serikali pamoja na mamlaka nchini Iran,” aliongeza. Mawasiliano yameanzishwa na Ofisi ya Maendeleo ya Kigeni na Jumuiya ya Madola ya Uingereza (FCDO) ili kutoa maoni.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.