Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika Mahmoud Ali YoussoufPicha: Amanuel Sileshi/AFP/Getty Images
Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika, Mahmoud Ali Youssouf, amekanusha vikali madai ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhusu mauaji ya kimbari dhidi ya Wakristo kaskazini mwa Nigeria.
Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Youssouf amesema hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa mauaji ya kimbari yamefanyika kaskazini mwa Nigeria.
Mwenyekiti huyo wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika ameeleza kuwa mtu anapaswa kufikiria kwa kina kabla ya kutoa matamko ya aina hiyo, akisisitiza kuwa waathiriwa wengi wa mashambulizi ya kundi la Boko Haram ni Waislamu na wala sio Wakristo.
Mapema mwezi huu, Rais Donald Trump aliiagiza Wizara ya Ulinzi ya Marekani kujiandaa kwa hatua za kijeshi endapo Nigeria itashindwa kukomesha kile alichokitaja kuwa mauaji ya Wakristo. Hata hivyo, hakutoa ushahidi mahsusi kuthibitisha madai hayo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.