Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi COP-30 unaofanyika katika mji wa Belem Para, Brazil.Picha: Igor Mota/ZUMA/picture alliance
Katika juhudi za kuhakikisha makubaliano ya kina kuhusu mabadiliko ya tabianchi, Brazil imeamua kuongeza muda wa mazungumzo katika mkutano wa mazingira wa COP30.
Brazil imetangaza kuongeza muda wa mazungumzo katika mkutano wa mazingira wa COP30, ili kutoa nafasi kwa mataifa kufikia makubaliano kuhusu tofauti zilizopo juu ya malengo ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na fedha zinazohitajika kutekeleza malengo hayo.
Mwanadiplomasia anayeongoza mazungumzo hayo, André Corrêa do Lago, amesema masuala nyeti yalitarajiwa kutatuliwa katika kikao cha Jumatano, lakini hilo halikufanikiwa.
Ameeleza kuwa mashauriano zaidi yanahitajika na hivyo muda wa mwisho wa kufikia mwafaka huo umesogezwa hadi Jumamosi.
Kwa kawaida, viongozi wa kisiasa hufika katika wiki ya pili na ya mwisho ya mazungumzo ya hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa ili kukamilisha makubaliano yaliyopendekezwa na wapatanishi katika siku za mwanzo.
Muungano wa Nchi Ndogo za Visiwa (AOSIS), ukiungwa mkono na mataifa mengine, unasisitiza umuhimu wa mkutano huo kushughulikia ahadi dhaifu za kupunguza utoaji wa hewa chafu.
Ahadi hizo zimechangia ongezeko la joto duniani kufikia kiwango cha nyuzi joto 1.5°C kilichowekwa katika makubaliano ya Paris, hali ambayo kwa sasa inaonekana kuwa vigumu kuepukika.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.