Wanaharakati wa kiasili wavamia mkutano wa COP30 Brazil

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Picha: Larissa Schwedes/dpa/picture alliance

Vyombo vya habari nchini Brazil vinaripoti kuwa wanaharakati wa kiasili wamelivamia eneo kunakofanyika Mkutano Mkuu wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa nchini humo.

Vyombo kadhaa vya habari vya Amerika Kusini vimewaonyesha waandamanaji wakivunja mlango na kukabiliana na maafisa wa usalama usiku wa kuamkia leo.

Wanaharakati hao wanapinga kuharibiwa kwa ardhi za mababu zao, ikiwemo ukataji wa miti katika misitu ya mvua.

Maandamano zaidi yamepangiwa kufanyika mwishoni mwa wiki. Maelfu ya wanaharakati wa kiasili wanawakilishwa pia katika mkutano huo mkuu wa Umoja wa Mataifa katika mji wa Belem.

Rais wa Brazil Inacio Lula da Silva amezitaja jamii za kiasili kama washirika muhimu katika mkutano wa mwaka huu wa COP30.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment