Mpasuko mpya wazuka kati ya rais na Waziri Mkuu Senegal

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Picha: John Wessels/AFP/Getty Images

Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye na waziri wake mkuu Ousmane Sonko wamelumbana leo kutokana na hatua ya kuachishwa kazi kwa mwandani wa waziri mkuu huyo.

Hii ndiyo ishara ya hivi karibuni kabisa inayoonesha nyufa katika uhusiano wa viongozi hao wawili.

Jioni ya jana, Jumanne, Rais Faye alisema kuwa amemuachisha kazi Aissatou Mbodj, kama mratibu i wa muungano wao wa kisiasa, kutokana na kile alichodai ni “masuala yanayoleta mgawanyiko.”

Hatua ya Faye kumuachisha kazi Mbodj inakuja siku chache baada ya Sonko kupinga hatua hiyo hadharani katika mkutano mkubwa wa hadhara katika Mji Mkuu, Dakar.

Chama cha muungano kinachoongozwa na Sonko, Pastef, kimetoa taarifa kikisema kuwa rais Faye hakuwa na mamlaka ya kumuachisha kazi Mbodj na wamemkataa aliyetangazwa kuichukua nafasi yake, waziri mkuu wa zamani Aminata Toure ambaye ni mshirika wa rais.

Faye alichaguliwa kuwa rais kutokana na ushawishi mkubwa wa Sonko, baada ya mahakama nchini humo kumpiga marufuku waziri mkuu huyo, kugombea urais.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment