UN waonya mamilioni kukumbwa na njaa duniani

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Picha: Gianluigi Guercia/AFP/Getty Images

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa leo yameonya kuwa mamilioni ya watu kote duniani huenda wakakumbwa na njaa.

Shirika la Chakula na Kilimo, FAO na lile la Chakula Duniani, WFP, yamesema kukatwa kwa ufadhili wa mashirika hayo kunaifanya hali ambayo tayari ni mbaya, kuwa mbaya zaidi.

Katika ripoti ya pamoja, mashirika hayo yamesema machafuko ndicho chanzo kikuu cha kukosekana kwa usalama wa chakula, katika nyingi ya nchi zilizotambuliwa kuwa kwenye hatari ya kukabiliwa na njaa.

Mashirika hayo yaliyo na makao yake mjini Roma yameziorodhesha Haiti, Mali, Palestina, Sudan Kusini, Sudan na Yemen kama nchi zilizo katika hali mbaya zaidi.

Miongoni mwa nchi zilizowekwa kwenye orodha ya “kutia wasiwasi mkubwa” ni Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Somalia, Nigeria, Chad, Burkina Faso, Afghanistan, Syria na Myanmar.

WFP linasema kupunguzwa kwa ufadhili kumelipelekea shirika hilo kupunguza misaada kwa wakimbizi na kusitisha miradi ya kutoa mlo mashuleni katika baadhi ya nchi.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment