Umoja wa Mataifa wataka uchunguzi kwa mauaji Tanzania

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Tanzania kuchunguza mauaji ya Oktoba.Picha: Salvatore Di Nolfi/KEYSTONE/dpa/picture alliance

Umoja wa Mataifa umetowa wito wa kufanyika uchunguzi kwa kile kinachoaminika kuwa vifo vya mamia ya watu waliokuwa wakiandamana kupinga uchaguzi wenye utata nchini Tanzania.

Mkuu wa Kamisheni ya Haki za Binaadamu ya Umoja huo, Volker Türk, alisema kumekuwa na jaribio la makusudi la kuficha ushahidi, kufuatia ripoti kwamba polisi walikuwa wakiichukuwa miili kutoka vyumba vya maiti na kuipeleka maeneo yasiyojuilikana.

Türk aliitaka serikali ya Tanzania kuiwachia miili hiyo na kuikabidhisha kwa familia zao kwa ajili ya maziko.

Chama kikuu cha upinzani, CHADEMA, kinadai kuwa watu wapatao 2,000 waliuawa kwenye siku tatu za maandamano kufuatia uchaguzi wa Oktoba 29.

Hadi sasa, serikali haijatowa idadi kamili ya vifo kwenye mkasa huo.

Tamko la Umoja wa Mataifa lilitaja “mamia ya watu wanaaminika kuuawa” lakini umesema haujaweza kuthibitisha idadi rasmi kutokana na hali ilivyo tete nchini Tanzania, ambako huduma za intaneti zilikatwa kwa siku sita baada ya uchaguzi. 

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment