Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Rais wa mpito wa Syria Ahmed al-SharaaPicha: Khalil Ashawi/REUTERS
Rais wa mpito wa Syria Ahmed al-Sharaa, anatarajiwa kukutana na rais wa Marekani Donald Trump leo katika ikulu ya White House.
Ziara ya al-Sharaa inajiri siku chache tu baada ya Marekani kuondoa vikwazo dhidi yake.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa rais wa Syria kuzuru Washington tangu taifa hilo lilipopata uhuru mwaka 1946.
Mazungumzo ya Trump na al-Sharaa yanatazamiwa kujikita kwenye Syria kujiunga na muungano unaoongozwa na Marekani dhidi ya wanamgambo wa Kundi linalojiita ‘Dola la Kiislamu’ IS.
Mnamo mkesha wa mkutano huo, serikali ya Damascus ilisema inaanza operesheni kubwa dhidi ya wanamgambo wa IS.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.