Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa mara ya kwanza amekiri kwamba wanaharakati wawili wa Kenya waliotoweka nchini mwake kwa muda wa wiki tano walikuwa wamekamatwa.
Mwezi uliopita, mashuhuda waliripoti kuwaona Bob Njagi na Nicholas Oyoo wakilazimishwa kuingia kwenye gari na watu ambao waliovalia sare baada ya tukio la kisiasa ambapo walikuwa wakimuunga mkono kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine.
Habari za kutekwa kwao zilithibitishwa Jumamosi lakini hadi kufikia wakati huo mamlaka ilikuwa imekanusha kuwa wanazuiliwa.
Katika mahojiano ya moja kwa moja Jumamosi jioni, Museveni aliwataja wanaharakat hao wawili kama “wataalamu wa ghasia” ambao walikuwa wamefungiwa kwenye ”jokofu kwa siku kadhaa.”
Museveni alikuwa akijibu swali kuhusu maandamano yaliyoongozwa na vijana katika taifa jirani la Tanzania.
Rais huyo ambaye ameongoza Uganda kwa miongo minne aliyashutumu makundi ya kigeni kwa kuchochea ghasia na kusema “wale watakaofanya mchezo huo hapa Uganda watakiona cha mtema kuni”.
Bila ya kutaja majina, aliongeza kuwa wanaharakati wawili wa Kenya waliachiwa huru baada ya kupigiwa simu na “baadhi ya viongozi wa Kenya” waliokuwa wakisinikiza kuachiwa kwao.
Siku ya Jumamosi, shirika la Vocal Africa lilithibitisha kuwa wanaharakati hao wawili walikuwa salama, na kwamba wako safarini kutoka Busia nchini Uganda kuelekea mji mkuu wa Kenya, Nairobi.
“Wacha wakati huu uashirie mabadiliko muhimu katika udumishaji wa haki za binadamu katika eneo la Afrika Mashariki mahali popote katika Jumuiya ya Afrika Mashariki,” shirika hilo liliandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram.
Jeshi la Uingereza kusaidia kulinda Ubelgiji baada ya uvamizi wa ndege zisizo na rubani

Wanajeshi wa Uingereza na vifaa vyao vinatumwa nchini Ubelgiji kusaidia kuimarisha ulinzi wa baada ya uvamizi wa ndege zisizo na rubani unazoshukiwa kutekelezwa na Urusi.
Mkuu mpya wa jeshi la Uingereza, Sir Richard Knighton, ameiambia BBC Jumapili akiwa na Laura Kuenssberg kwamba mwenzake wa Ubelgiji aliomba usaidizi mapema wiki hii na vifaa hivyo na wafanyakazi wako njiani kuelekea huko.
Uwanja mkuu wa ndege wa Zavantem nchini Ubelgiji ulilazimika kufungwa kwa muda Alhamisi usiku baada ya ndege zisizo na rubani kuonekana juu ya anga lake.
Ndege hizo iiazilionekana katika maeneo mengineya nchi, ikiwa ni pamoja na kambi ya kijeshi.
Sir Richard alisema haijulikani ikiwa uvamizi huo ulikuwa wa Urusi, lakini akaongeza kuwa kuna “unawezekana” zilikuwa zinatekeleza amri ya Moscow.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.