Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Maafisa nchini Marekani wanatathmini iwapo watawasilisha mashtaka dhidi ya mwenye nyumba wa Indiana ambaye alimpiga risasi na kumuua mjakazi ambaye alibisha kimakosa nyumba isiyo sahihi.
Polisi wanasema walimpata Maria Florinda Rios Perez akiwa amekufa mbele wa nyumba hiyo siku ya Jumatano muda mfupi kabla ya 0700 saa za ndani (12:00 GMT).
Awali polisi walikimbilia eneo la tukio baada ya wenyeji kupiga ripoti kuhusu uwezekano wa uvamizi kwenye kitongoji cha Indianapolis cha Whitestown.
Wawili hao hawakuonekana kuingia ndani ya nyumba hiyo, polisi walisema kwenye taarifa.
Wamewasilisha kesi hiyo rasmi kwa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Kaunti ya Boone ili ikaguliwe ili kubaini iwapo mashtaka ya uhalifu yataanziswa rasmi.
Polisi hawajatoa majinia ya watu waliokuwa ndani ya nyumba hiyo au mtu aliyefyatua risasi, wakisema katika taarifa siku ya Ijumaa kwamba ni “suala lenye utata ambalo bado linaendelea, ni hatari kutoa maelezo zaidi kuhusu tukio hilo”.
Walihimiza uvumilivu, wakionya “kuhusu kuenea kwa habari potofu mtandaoni” kuhusu kesi hiyo.
Mauricio Velazquez, aliiambia CBS News, mshirika wa BBC wa Marekani, kwamba anatapigania haki ya mke wake mwenye umri wa miaka 32.
Taarifa zaidi zinasema alikuwa mama wa watoto wanne na asili yake ni Guatemala.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.