Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Rais wa Marekani, Donald TrumpPicha: Jonathan Ernst/REUTERS
Rais wa Marekani Donald Trump, amesema hakuna afisa wa Marekani atahudhuria mkutano wa kilele wa G20 utakaofanyika Afrika Kusini, kwa madai yasiyo na ushahidi ya “kuuawa na kuchinjwa” kwa raia wa kizungu.
Kupitia chapisho kwenye mtandao wake wa Truth Social, Trump amesema ni aibu kubwa kwamba mkutano huo unafanyika Afrika Kusini wakati ukiukwaji huo wa haki za kibinadamu unaendelea.
Pia ameongeza kuwa Waafrika hao Wazungu ambao ni vizazi vya walowezi wa kwanza wa Kizungu nchini Afrika Kusini wanauawa na kuchinjwa, pamoja na ardhi na mashamba yao kutwaliwa kinyume cha sheria.
Trump anatazamia kuandaa mkutano wa G20 wa mwaka 2026
Rais huyo amesema anatazamia kuandaa mkutano wa kilele wa G20 wa mwaka 2026 nchini Marekani katika eneo lake binafsi la mapumziko la kuchezea gofu huko Miami, Florida.
Kwa upande wake, wizara ya mambo ya nje ya Afrika Kusini, imeyataja matamshi ya Trump kuwa ya “kufadhaisha” na kusema inatazamia kuandaa mkutano “wenye mafanikio” utakaofanyika Novemba 22-23.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.