Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Ghasia za uchaguzi nchini Tanzania mnamo Oktoba 30, 2025Picha: Thomas Mukoya/REUTERS
Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Tanzania yamelaani ripoti zilizoenea za mauaji ya dhidi ya raia, baadhi majumbani mwao, katika ghasia za baada ya uchaguzi.
Katika taarifa ya pamoja na mashirika mengine sita yasiyo ya kiserikali, Kituo cha Sheria na Haki za Kibinadamu (LHRC) kimesema kulikuwa na “matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji wasio na silaha.
LHRC pia imesema familia zimeachwa zikiwa na kiwewe, na watoto wameshuhudia ukatili dhidi ya wazazi wao.
Vijana ndio waliolengwa katika ghasia nchini Tanzania
Taarifa hiyo imeendelea kusema vijana hasa ndio waliokuwa walengwa na kwamba mamia ya watu wamekamatwa, wengine wakisalia kizuizini bila dhamana.
Imeonya kuwa kiwango cha ukiukwaji wa haki za binadamu bado hakijafichuliwa kikamilifu, ikikosoa kukatizwa kwa mtandao na vikwazo dhidi ya vyombo vya habari.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.