Rutte akusudia kuangazia uwezo wa nyuklia wa NATO

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Katibu mkuu wa jumuiya ya kujihami ya NATO, Mark RuttePicha: Piroschka Van De Wouw/REUTERS

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami, NATO, Mark Rutte, amesema katika siku zijazo, anakusudia kuangazia zaidi uwezo wa nyuklia wa muungano huo wa ulinzi wa nchi za Magharibi, kama kingi dhidi ya kitisho kutoka Urusi.

Kwenye maoni katika toleo la Jumapili la gazeti la Die Welt yalioonekana mapema na shirika la habari la dpa, Rutte amesema ni muhimu kuzungumza zaidi na jamii zao juu ya uwezo wa kuzuia kitisho cha silaha za nyuklia, ili kuhakikisha zinaelewa jinsi suala hilo linavyochangia kwa ujumla katika usalama wao.

NATO yasema ina kinga dhidi ya matumizi ya nyuklia

Ameongeza kusema wakati Urusi inatumia matamshi hatari na ya kiholela kuhusu nyuklia, raia wao hawapaswi kuwa na hofu kwa sababu NATO ina kizuizi kikali dhidi ya matumizi ya nyuklia ili kulinda amani, kuzuia kushurutishwa na uchokozi.

Rutte pia amesema uwezo wa nyuklia wa NATO ni dhamana ya mwisho ya usalama wao na muhimu na kwamba unapaswa kubaki kuwa wa kuaminika, salama na unaofaa.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment