ICC yathibitisha mashtaka dhidi ya Joseph Kony

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Mbabe wa kivita wa Uganda, Joseph KonyPicha: Stuart Price/epa/dpa/picture alliance

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, jana Alhamisi ilithibitisha mashtaka yote 39 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu yanayodaiwa kufanywa na mbabe wa kivita wa Uganda, Joseph Kony.

Majaji wa mahakama hiyo wamesema kuna sababu za kutosha kuwa Kony alihusika na mashtaka 29 kama mhusika asiye wa moja kwa moja.

Makosa yanayohusishwa na Kony

Haya yanahusiana na mashambulizi yaliofanywa na kundi la waasi wa Lord’s Resistance Army, LRA,  dhidi ya shule na kambi za wakimbizi wa ndani ikiwa ni pamoja na mauaji, mateso, ndoa za lazima, mimba za kulazimishwa, ubakaji, na kuwasajili jeshini watoto walio na umri wa chini ya miaka 15.

Mahakama hiyo ya ICC pia imesema Kony alikuwa na kesi ya kujibu kama mhusika wa moja kwa moja katika kesi 10 zinazohusiana na waathiriwa wawili waliolazimishwa kuwa wake zake.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment