Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon kimeyakosoa mashambulizi ya Israel kusini mwa LebanonPicha: Marwan Naamani/dpa/picture alliance
Jeshi la Israeli limesema kuwa limekamilisha mashambulizi dhidi ya maeneo ya kijeshi ya kundi la wanamgambo wa Hezbollah kusini mwa Lebanon.
Jeshi la Israeli lilisema vikosi vyake viliyalenga maghala ya silaha kutoka kitengo cha juu cha Radwan cha wanamgambo hao wa Hezbollahwanaoungwa mkono na Iran, vikilishutumu kundi hilo kwa kujipanga upya kinyume na makubaliano ya kusitisha mapigano.
Kabla ya mashambulizi hayo, IDF iliwataka wakazi kuondoka katika majengo fulani na mazingira yake katika maeneo matano kusini mwa nchi. Kulingana na shirika la habari la serikali NNA, Rais wa Lebanon Joseph Aoun alieleza mashambulizi hayo kama “uhalifu mkubwa” uliofanywa na Israeli.
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa hapo jana waliyalaani mashambulizi hayo, wakiyaita kuwa ni ukiukwaji wa wazi wa azimio la Baraza la Usalama nambari 1701 na kuonya kwamba hatua za kijeshi “zinadhoofisha maendeleo yanayofanywa kuelekea suluhisho la kisiasa na kidiplomasia.
Taarifa kutoka kwa Kikosi cha Muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon (UNIFIL) ilisema iliitaka Israeli kusitisha mara moja mashambulizi haya na ukiukwaji wote wa azimio nambari 1701.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.