Ulaya, Marekani kusaidia usambazaji nishati kwa Ukraine

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Ujumbe wa Marekani katika mkutano kuhusu msaada wa nishati kwa Ukraine huko Athens, UgirikiPicha: Thanassis Stavrakis/AP Photo/picture alliance

Mawaziri wa nishati wa Marekani na Ulaya wanafanya mazungumzo nchini Ugiriki Alhamisi 06.11.2025 juu ya namna ya kusaidia usambazaji wa nishati kwa Ukraine hasa wakati msimu wa baridi kali ukikaribia.

Juhudi hizo zinafanyika wakati ambapo Rais wa Marekani Donald Trump anajaribu kuushinikiza Umoja wa Ulaya ununue gesi kutoka Marekani. Mkutano huo unafanyika wakati Urusi na Ukraine zikiendelea kupambana. Jeshi la Ukraine limesema limeulenga mtambo wa kusafisha mafuta wa Volgograd wa Urusi na kusababisha kifo cha mtu mmoja.

Mmoja auwawa kwa mashambulizi ya droni Urusi

Gavana Andrei Bocharov amesema mtu huyo ameuawa kwa kuangukiwa na mabaki ya droni yaliyosababisha moto mkubwa katika eneo la viwanda wakati vikosi vya Urusi  vinaendelea kusonga mbele Kaskazini mwa Pokrovsk nchini Ukraine kwa lengo la kuudhibiti kikamilifu mji huo.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment