HAYA NI MAMBO 5 YALIYOTUFUNZA KUHUSU MAISHA.

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Kipindi cha Lockdown:

Poleni sana watanzania wenzangu kwa kupoteza biashara,ndugu au watu wa karibu katika kipindi cha mpito.

Wakati lockdown wengi wamepitia changamoto hasa katika mambo kadhaa
Hili ni FUNZO ambalo wengi wamejifunza na unahitaji kujua na kuchukua hatua…

1. MAISHA YANAHITAJI KUWA NA AKIBA .


Sio kutumia kila pesa unapaswa iishie Kwenye matumizi hujui kesho yako ni nini.?
Watu Walioweza kuishi bila msongo ni wale ambao walikuwa na pesa za akiba na sio wengine.
Kama Umeteseka katika hicho pole sana ni wakati wa kujifunza na kuchukua hatua. Akiba ni ukombozi wa kipindi cha shida.

2.NIDHAMU YA PESA


Watu walikuwa wanaheshimu pesa hata 1000 ilikuwa inapewa nidhamu..
Mtu alikuwa hawezi kutoa pesa bila sababu ya msingi, pesa ilitumika katika vitu ambayo ni vya muhimu na sio show off ..
Hivyo ndivyo unahitaji kila siku kwenye maisha yako USITUMIE pesa vibaya ili kuweza kufika mbali …

3. MTU ALIKUWA TAYARI KULA CHOCHOTE ILI AWEZE KUSHIBA NA KUISHI.


Watu hawakujali kama kuna kuchafua meza na wengine kuna vyakula walikuwa HAWALI ila kipindi Cha Lockdown walikula ..
Kumbe unaweza kuishi bila kufanya hivyo hata nyakati zingine kwa MALENGO maalumu ili kuvuka kwenda hatua ya juu.

4. KUDUMISHA MAHUSIANO.


Wengi walikuwa na familia zao pamoja wakapata muda mzuri wa kukaa pamoja kwa sababu ya lockdown kwani siku zingine walikuwa busy katika biashara
Unahitaji kwenye maisha kupata muda wa kukaa na familia au ndugu zako wa karibu ili kudumisha mahusiano yako.

5.KUPATA MUDA WA KUPUMZIKA.


Wengi walipata muda wa utulivu wa kuresh akili na kujenga Afya .
Mwili unahitaji kupumzika, hatakuja kusikia filimbi ikisema sasa unahitaji kupumzika.Jipe muda binafsi wa kupumzika.

Usisubiri kupata shida kama hizi wakati wa majanga..Pata FUNZO hili 

Umejifunza nini na kitu gani unahitaji kukifanyia kazi ili usiteseke wakati wa majanga kama haya..?

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment