Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Maafisa wa jeshi la Uganda na DRC katika operesheni Beni mnamo Desemba 9, 2021Picha: Alain Uaykani/Xinhua News Agency/picture alliance
Vikosi vya usalama nchini Uganda vimesema kuwa vimemuua mganga mmoja kwa jina Christian Asuman Muganzi, anayedaiwa kuongoza mashambulizi ya kuratibiwa wikendi iliyopita dhidi ya vituo vya polisi na jeshi .
Afisa wa jeshi huko Bundibugyo Albert Kaliruga, ameliambia shirika la habari la AFP kuwa Muganzi aliongoza kundi linalotaka kuchukua silaha ili kuanzisha uasi wa kikabila, lakini kwamba limerudishwa nyuma na vikosi vya usalama.
Wapiganaji 20 wauawa na 15 kukamatwa
Kaligura amesema Muganzi alizingirwa kwenye maficho yake huko Kakuka, Bundibugyo hapo jana na kuuawa pamoja na zaidi ya wapiganaji wake 20, huku wengine 15 wakikamatwa.
Kaligura ameongeza kusema Muganzi alikuwa akitumia madhabahu yake ya kitamaduni kuwasajili na kuwafunza wapiganaji wake pamoja na kutumia dawa za mitishamba na imani za kishirikina ili kuwalinda wakati wa vita.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.