Hamas yakabidhi mwili wa mateka mwingine kwa Israel

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Maafisa wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu wapokea miili ya Wapalestina 45 waliokuwa wakishikiliwa na IsraelPicha: Abed Rahim Khatib/Anadolu/picture alliance

Mabaki ya mateka yaliokabidhiwa kwa Israeli na kundi la Hamas jana jioni yametambuliwa kuwa ya mwanajeshi aliyetakwa nyara mnamo Oktoba 7, 2023. Haya yamesemwa mapema leo na jeshi la Israel.

Kupitia taarifa kwenye mtandao wa Telegram, jeshi hilo limesema kuwa mabaki hayo yalikuwa ya Itay Chen mwenye umri wa miaka 19, mwanajeshi mwenye uraia pacha wa Marekani na Israel ambaye pia alikuwa na uraia wa Ujerumani.

Jeshi hilo pia limesema Chen aliuawa wakati wa mapigano katika eneo la Kibbutz Nir Oz, na kwamba kifo chake kilithibitishwa rasmi mnamo Machi 10, 2024.

Chen alikuwa mateka wa mwisho mwenye uraia wa Marekani na Israel aliyesalia katika Ukanda wa Gaza.

Mabaki ya Chen yalikabidhiwa kwa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu na baadaye kusafirishwa kwa taasisi ya ukaguzi wa kimatibabu nchini Israel kwa utambuzi.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment