Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Picha: Yves Herman/REUTERS
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ametoa mwito kwa Rais Viktor Orban wa Hungary kuacha kupinga ombi la nchi yake kujiunga na Umoja wa Ulaya.
Zelenskiy ameyasema haya wakati ambapo Umoja wa Ulaya unaunga mkono kuisogeza Ukraine hatua moja zaidi kuelekea kujiunga na umoja huo licha ya hofu za ufisadi uliokithiri nchini humo.
Hatua ya Urusi kuivamia Ukraine imeleta azma mpya ya Umoja wa Ulaya kutaka kusajili wanachama wapya.
Kwa sasa nchi kumi zinataka kujiunga na umoja huo ulio na mkataifa 27.
Brussels inasema upo uwezekano wa wanachama wapya kujiunga katika miaka ya hivi karibuni. Mbali na Ukraine, Montenegro, Albania na Moldova zimewasilisha maombi yao ya kutaka kujiunga.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.