Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Picha: Bahho Kara/Kirchner-Media/IMAGO
Winga wa Bayern Munich Luis Diaz alifunga mabao mawili ya kipindi cha kwanza na kuisaidia timu yake kuwalaza mabingwa watetezi Paris Saint Germain 2-1.
Mechi hiyo ya Ligi ya Vilabu Bingwa barani Ulaya ilichezwa mjini Paris katika uwanja wa Parc des Princes.
Diaz lakini alionyeshwa kadi nyekundu muda mfupi baada ya kufunga goli la pili baada ya kumchezea vibaya Achraf Hakimi. Joao Neves aliwapa PSG bao la kufutia machozi mnamo kipindi cha pili.
Timu nyengine ya Ujerumani Eintracht Frankfurt iliwazuia mabingwa wa Italia Napoli sare ya kutofungana.
Katika mechi nyengine muhimu usiku wa kuamkia leo Liverpool waliwalaza Real Madrid 1-0 uwanjani Anfield Alexis Mcallister akiwa mfungaji wa goli hilo la pekee.
Leo hii Borussia Dortmund watakuwa mjini Manchester kukwaana na Manchester City.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.