Peru yavunja mahusiano ya kidplomasia na Mexico

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Picha: Guadalupe Pardo/AP Photo/picture alliance

Serikali ya Peru imesema imevunja mahusiano ya kidplomasia na Mexico kwa kuwa nchi hiyo imempa hifadhi waziri wake mkuu wa zamani.

Waziri huyo mkuu wa zamani Betssy Chavez, anachunguzwa kwa madai ya kuhusika katika jaribio la mapinduzi la mwaka 2022 lililofanywa na rais wa zamani Pedro Castillo.

Akizungumza na waandishi wa habari, waziri wa mambo ya kigeni wa Peru, Hugo de Zela, mbali na kumpa hifadhi Chavez, serikali ya peru imechukua hatua hiyo kwa kuwa Mexico imekuwa ikiingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo.

Peru ilimfukuza nchini humo balozi wa Mexico baada ya Mexico kumpa hifadhi mke wa rais wa zamani wa Peru Pedro Castillo na watoto wake.

Castillo anakanusha mashtaka ya kufanya jaribio la mapinduzi akisema hakubeba silaha dhidi ya nchi yake kwasababu jeshi lilikataa kutii amri zake.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment