FURSA YA BIASHARA YA KILIMO KWA SASA.

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Watu wengi bado wanaona kilimo kama kazi ya kijijini, ilhali ukweli ni kwamba kilimo ni biashara yenye mzunguko mkubwa wa fedha duniani.
Kuali maarufu inasema ” Kilimo ni utimgongo wa taifa.” Kwani

✅

 Kinaongeza usalama wa chakula

✅

 Kinatoa ajira

✅

 Kinakupa uhuru wa kifedha.

Fikiria hivi…


Unapotumia mbegu bora, mbinu sahihi, na masoko yenye uhakika, shamba lako linaweza kukupa faida zaidi ya ofisi yoyote uliyowahi kuota.

Hii ndiyo fursa ya leo,
Anza kuangalia bidhaa gani sokoni zina mahitaji makubwa lakini upatikanaji mdogo.
Kuanzia mboga mboga, matunda, mimea ya dawa, hadi ufugaji wa kisasa. Kila moja ina nafasi yake ya kukupa mapato makubwa.

Jinsi ya kutengeneza fursa kwenye kilimo.


1.Fanya kilimo cha mboga mboga (nyanya, pilipili, vitunguu nk) kinaweza kuanza na Tsh 500,000 – 5,000,000 kulingana na ukubwa wa shamba na mbinu (kawaida au kisasa).

2. Fanya kilimo cha matunda (parachichi, maembe,kokoa,ndizi, nanasi nk) mara nyingi kinahitaji mtaji wa Tsh 2M – 10M kwa maandalizi ya shamba, miche, na utunzaji.

3.Fanya kilimo cha mazao makubwa (mahindi, mpunga, mihogo,karanga, maharage,soya nk.) kinaweza kuanzia Tsh 1M – 10M kwa msimu kulingana na ukubwa wa eneo.

4. Fanya ufugaji
Fuga kuku, ng’ombe, mbuzi n.k kulingana na eneo lako na uwezo wako mtaji kuanzia 50,000 – 5,000,000/=

5. Nunua mazao na uza kwa faida.
Unaweza ukawa unanunua kwa wakulima na kuuza kwa wateja au katika soko, nunua msimu wa mavuno, utapiga sana hela.

Ukweli wa msingi ni kuwa matokeo makubwa kwenye kilimo si tu kuhusu kiasi cha mtaji, bali ni mchanganyiko wa mtaji + maarifa + soko + nidhamu ya uendeshaji mavuno yako yatakuwa ushuhuda.

Unahitaji kupata maarifa zaidi ya kilimo gani.?Niandikie hapa chini Kwenye comment niweze kukusaidia.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment