Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Takaichi kuzungumza na Kim kuhusu utekaji wa raia wakePicha: Kim Kyung-Hoon/REUTERS
Waziri Mkuu wa Japan Sanae Takaichi ametuma ombi la kuzungumza na rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, kusawazisha mvutano wao wa muda mrefu kuhusu utekaji wa raia wa Japan uliofanywa na Pyongyang miongo iliyopita.
Takaichi amesema ili kujenga uhusiano ulio wa wazi na wakuaminiana, ni lazima akutane ana kwa ana na Kim Jong Un, kujadili suala hilo. Bado utawala wa Kim haujasema chochote kuhusu ombi hilo.
Viongozi wa zamani wamejaribu kuwa na mazungumzo na Kim kuhusu utekaji huo lakini juhudi zao hazikufua dafu.
Baada ya miaka mingi ya kukanusha madai hayo, mwaka 2002, Korea Kaskazini ilisema maafisa wake waliwateka nyara raia 13 wa Japan miaka ya 70 na 80, waliotumika kuwapa mafunzo ya lugha na tamaduni za kijapani wapelelezi wa Korea Kaskazini.
Hata hivyo Japan inaamini raia wake waliotekwa wanafikia 17 huku maafisa wengine wakisema idadi hiyo inaweza kuwa kubwa zaidi.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.