Ukatili wa El Fasher huenda ukawa uhalifu wa kivita

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICCPicha: Piroschka van de Wouw/REUTERS

Ofisi ya Mwendesha mashitaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, imeonya kuwa ukatili unaofanyika katika mji wa El Fasher Sudan, unaweza kuchukuliwa kuwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinaadamu.

Ofisi ya Mwendesha mashitaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, imeonya kuwa ukatili unaofanyika katika mji wa El Fasher Sudan, unaweza kuchukuliwa kuwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinaadamu.

Ofisi hiyo imesema ina wasiwasi kuhusu mauaji ya halaiki, ubakaji na uhalifu mwengine unaodaiwa kufanyika katika mji huo ulioko katika mkoa wa Darfur Magharibi.

Baada ya miezi 18 ya kuuzingira mji huo, mashambulizi na njaa kali, wanamgambo wa RSF waliudhibiti Oktoba 26 baada ya kuwa mikononi mwa vikosi vya usalama. El Fasher ndio ngome ya mwisho kubwa zaidi iliyokuwa inashikiliwa na vikosi hivyo.

Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya watu 65,000 wameukimbia mji huo, huku wengine 5000 wakihamia katika mji jirani wa Tawila lakini maelfu ya wengine wengi bado wamekwama katika mji huo unaokumbwa na vita.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment